Home Siasa POLEPOLE AWASHANGAA WAPINZANI WANAOBEZA MIRADI YA MAENDELEO ILIFANYWA NA SERIKALI YA AWAMU...

POLEPOLE AWASHANGAA WAPINZANI WANAOBEZA MIRADI YA MAENDELEO ILIFANYWA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

0

………………………………………………………………………………..

NA FARIDA SAIDY, MOROGORO

Baada ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhitimisha Bunge la kumi { 11 } hapo jana Juni 16, Umoja wa vijana wa vyuo vikuu mkoa wa Morogoro, Umetoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na Serikali ya awamu ya tano kwa ujumla kwa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.

Katika Kongamano hilo la pongezi lililoongozwa na mlezi wa wanafunzi wa vyuo vikuu ambaye pia ni katibu mwenezi wa CCM Bw. Humphrey Polepole, amesema Serikali ya awamu ya tano imetekeleza ilani ya chama kama walivyoahidi katika uchaguzi ulipita wa mwaka 2015.

Hata hivyo amesema pamoja na utekelezaji wa miraadi mbalimbali ya maendeleo kwa watanzania, pia Serikali ya awamu ya tano inawatoa hofu wananchi na kuendelea na maisha yao ya kawaida kwan imefanikiwa kupambana na kuudhibiti ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virus vya corona, ugonjwa ambao unaitesa dunia kwa sasa .

Aidha Humphrey Polepole ameshangazwa na namna ya upinzani wa vyama vya siasa nchini katika kupinga miradi ambayo inafaida kubwa na maslahi mapana kwa wananchi na taifa kwa ujumla katika kukuza uchumi.

Katika hatua nyingine Polepole amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu kwa kuwachagua viongozi ambao wapo tayari kuwasaidia na kuwatatulia matatizo yao kwa wakati baada ya uchaguzi na sio viongozi wenye tamaa ya madaraka.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi waliohudhuria mkutano huo akiwepo mwenyekiti wa vijana CCM Mkoa wa Morogoro Ramadhan Kimwaga amedai pamoja na Mheshimiwa Rais kuchukua fomu ya Urais lakini anaungana hoja za baadhi ya waliokua wabunge wa Bunge la Jamhuri kwa upande wa chama tawala kwa kutokuchukua fomu za kugombea nafasi ya urais ili kumuunga mkono Mheshimiwa Rais.