Jengo la mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba
********************************
Na Masanja Mabula ,Pemba.
HUKUMU ya kesi ya udhalilishaji inayomkabili Abdalla Faki Ali 22 iliyokuwa itolewe leo katika mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imeahirishwa kutokana na hakimu wa mahakama hiyo kuwa nje ya ofisi kikazi.
Ktuhumiwa huyo ambaye anakabiliwa na kesi ya ubakaji anadaiwa kutenda kosa hilo terehe 10/09.2019 huko Limbani Wilaya ya Wete.
Kesi hiyo imeahirishwa katika mahakama ya Mwanzo Wete , chini ya Hakimu wa mahakama hiyo Maulid Ali Hamad , ambapo Mwendesha mashtaka koplo Khamis Mzee alitaka ipangiwe siku nyengine kwa ajili ya kusikilizwa.
“Mhe Hakimu kesi hii inasikilizwa katika mahakama ya Mkoa , lakini kutokana na hakimu wa mahakama hiyo kutokuwapo , naomba upange siku nyengine”alisema.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo ikiwa ni kinyume na kifungu cha 108 (1) ,(2) ,(e) na 109 (1) vya sheria namba 6/2018 , sheria ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hivyo mtuhumiwa huyo amerejeshwa rumande hadi tarehe 29/06/2020 kesi yake itakapo kuja kutajwa katika mahakama ya Mkoa.