Home Mchanganyiko WAZIRI NDALICHAKO AWEKA WAZI RATIBA YA MIHULA NA MITIHANI YA TAIFA

WAZIRI NDALICHAKO AWEKA WAZI RATIBA YA MIHULA NA MITIHANI YA TAIFA

0

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma wakati akitangaza  rasmi tarehe za mitihani ya taifa kwa watahiniwa wa Mwaka 2020 na mihula ya masomo kwa shule zote nchini zitakazoanza June 29 mwaka huu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo kwa   waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma wakati akitangaza  rasmi tarehe za mitihani ya taifa kwa watahiniwa wa Mwaka 2020 na mihula ya masomo kwa shule zote nchini zitakazoanza June 29 mwaka huu

……………………………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ametangaza rasmi tarehe za mitihani ya taifa kwa watahiniwa wa Mwaka 2020 na mihula ya masomo kwa shule zote nchini.

Prof. Ndalichako ametangaza hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Rais,wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuelekeza shule zote kufunguliwa tarehe 29 Juni mwaka hu una shughuli nyingine kuendelea baada ya kuona mwenendo wa janga la corona linapungua nchini.

Akizungumza Prof. Ndalichako amesema kuwa Ratiba za Mitihani itakuwa Darasa la saba (PSLE) 07/10/2020 mpaka 08/10/2020, kidato cha pili (FTNA)09/11/2020 mpaka 20/11/2020, kidato cha nne(CSEE)23/11/2020 mpaka 11/12/2020 na darasa la nne (SFNA)25/11/2020.

Aidh Prof. Ndalichako amesema kuwa kwa shule za msingi na sekondari wanafunzi watarejea shuleni tarehe 29 Juni, 2020 na kumaliza muhula wa kwanza wa masomo tarehe 28 Agosti,2020 na kuanza muhula wa pili ambao utaisha 18 Desemba 2020.

Prof. Ndalichako amesema kwa wanafunzi wa kidato cha tano wataripoti shuleni 29 Juni 2020 kama ilivyotangazwa na watasoma na kukamilisha muhtasari wa kidato cha tano  na mitihani iifikapo tarehe 24 Julai,2020, wanafunzi wataanza rasmi masomo ya kidato cha sita tarehe 27 Julai,2020.

Kwa kuongezea Prof. Ndalichako amesema kuwa Wizara inapenda kusisitiza uongozi wa shule zote nchini kuhakikisha wanafunzi , walimu na wafanya kazi wasio walimu wanazingatia maelekezo ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kama yalivyotolewa na Wizara ya Afya .

“Hii ni Pamoja na kuhakikisha kuwa shule zinanunua vifaa vya kutosha kwa ajili ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni”, ameelekeza Prof. Ndalichako.

Prof. Ndalichako amesema Ili kukamilisha muhtasari wa masomo shule zitalazimika kuongeza saa mbili za masomo kwa siku ili kufidia muda uliopotea.

Natoa wito kwa walimu na wanafunzi kuhakikisha wanajituma katika ufundishaji na ujifunzaji ili kukamilisha mihtasari kwa muda uliopanga na kwa mafanikio,” ametoa wito Prof. Ndalichako