Home Mchanganyiko ”USHIRIKIANO WA WATANZANIA KATIKA UTENDAJI WANGU UMELETA CHACHU YA MAENDELEO NDANI YA...

”USHIRIKIANO WA WATANZANIA KATIKA UTENDAJI WANGU UMELETA CHACHU YA MAENDELEO NDANI YA MIAKA MITANO” -RAIS DKT.MAGUFULI

0

……………………………………………………………..

Na. Alex Sonna, Dodoma

Serikali imesema kutokana na utendaji bora na utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini ni ushuhuda tosha kuwa watendaji wote kwa kushirikiana na wabunge bila kusahau wanachi kila mmoja katika nafasi yake katimiza wajibu wake ndo maana ya matokeo chanya ya maendeleo yaliyopatikana nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo wakati  kulihutubia bunge ili kufunga shughuli za kibunge.

Aidha Rais Magufuli amewapongeza madiwani wote nchini kwa utendaji bora katika kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo yao ili kufikia matokeo chanya yanayotakiwa kufikiwa kwa wananchi wao.

Rais Magufuli amewashukuru watangulizi wake kwa kuaanda mazingira Rafiki ya yeye kutimiza na kufanyikisha maendeleo yaliyopangwa kwa watanzania.

“Utendaji na mafanikio yote tuliyofikia katika kipindi cha miaka mitano ni kutokana na ushirikiano wenu wabunge na kuonyesha uimara wa bunge hili tukufu”, ameeleza Rais Magufuli