Home Mchanganyiko UNODC YAIPONGEZA TANZANIA KWA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

UNODC YAIPONGEZA TANZANIA KWA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

0

…………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Tanzania imefanikiwa kuvunja mitandao ya biashara ya dawa za kulevya kwa asilimia 90 hiyo ni kutokana na taarifa ya UNODC waliyotoa hivi karibuni.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakati akilihutubia bunge pamoja na kufunga shughuli za kibunge.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa serikali imefanikiwa kudhibiti mitandao ya kusafirisha dawa za kulevya na hiyo inatokana na utendaji bora wa wafanya kazi na hii ni ishara tosha kuwa vitendo vya rushwa vilivyokuwa vinafanyika  katika mipaka na viwanja vya ndege imekomeshwa.

Rais Magufuli amesema kuwa uadilifu katika utendaji wa wafanya kazi nchini umeimarisha ukusanyaji wa mapato na kuleta ongezeko kubwa la makusanyo yanayopatikana.