*******************************
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mchezo wa Karate imeanza Tena mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki mashindano ya Dunia ya Karate huko Japani Mwaka ujao.
Mashindano hayo ya Karate ya Dunia yalikuwa yafanyike mwezi octoba mwaka huu ,lakini yakaahilishwa kutokana na Tahadhari ya Virusi vya Corona.
Michuano hiyo huwa inafanyika kila baada ya Miaka 3,na wakati huu Tanzania pia imepata nafasi ya Kipekee kwa kutoa Jaji wa michuano hiyo ambaye ni (Sensei)Jerome Mhagama..
Tumezungumza Jerome Mhagama ambaye Pia ni Mkufunzi mkuu wa Karate Tanzania Juu ya nafasi hiyo iliyopata nchi ya Tanzania.
VIDEO- Jerome mhagama -Mkufunzi mkuu wa karate Tanzania.mp4
Haya ni mashindano ya 15 ya Dunia Tangu kuanzishwa kwake,na Tanzania imewahi kushiriki mara Mbili katika mashindano hayo. Kwa mara ya kwanza mwaka 2011 mashindano hayo yaliyofanyika Nchini Tailand,Tanzania Ilipeleka mchezaji mmoja ambaye alifika katika hatua ya 16 Bora.
Mwaka 2014 Katika mashindano yaliyofanyika Japan Tanzania Ilishiriki katika mashindano hayo kwa Kupeleka Jaji .