**********************************
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
BAADHI wataalamu wa kilimo na mifugo Kibaha,Pwani wamesema bajeti iliyopendekezwa imegusa maslahi ya Mtanzania licha ya kutoa maoni yao kuwa yapo maeneo hayajaguswa kumnufaisha mkulima wa kisasa ikiwemo wataalamu wa ugani wasajiliwe ili kwenda sambamba teknolojia ya kisasa katika kilimo pamoja na kujenga viwanda vingi vya mbolea ndani ya nchi .
Aidha upande wa suala la uboreshaji wa kilimo kwa kuweka mazingira ya upatikanaji wa vifaa vya kilimo kwa gharama nafuu ikiwa ni pamoja na mashine na vipuri vya kilimo .
Akitoa maoni yake kuhusu bajeti iliyowasilishwa bungeni Juni 11,mwaka huu mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi 2020/2021 ambapo serikalu imepanga kutumia sh.trilioni 34.9 kwa matumizi ya maendeleo, ofisa mstaafu wa mifugo na mkurugenzi wa shamba darasa Kibaha ,mkoani Pwani, Ephrahim Masawe alisema ,wakati wakulima wakikimbilia soko la dunia mambo hayo yanapaswa yagusiwe.
Alibainisha ,kwasasa nchi ikihimiza kilimo cha kisasa na kuondokana na jembe la mkono , wataalamu wa ugani wanatakiwa wasajiliwe kama ilivyo kwa madaktari wa mifugo ama binadamu ili wawe na umoja wao unaotambulika .
Masawe alielezea ,kilimo kibadilike ili kiwe kidigital na teknolojia ya kisasa kwa lengo la kuhamasisha Tanzania ya viwanda ni lazima kuwe na kilimo na viwanda vinavyolandana na udigital .
“Mbolea nyingi inaagizwa nje ya nchi ,ni wakati wa kujenga viwanda vingi nchini kwetu ” Uboreshaji wa kilimo kwa kuweka mazingira ya upatikanaji wa vifaa vya kilimo kwa gharama nafuu yakiwemo matrekta, vilainishi vya mitambo ya kilimo, mashine za kupulizia dawa na mashine za kukamulia mafuta ya alizeti, ufuta, karanga, chikichi na karanga”:;alisema Masawe .
Kuhusu viatilifu ,anasema vinatumika mara kwa mara pamoja na vifaa vyake kwenye pamba, korosho ,kahawa ,alizeti bajeti ieleze kama Jana ruzuku na itamke wazi kama tozo la kodi zimeondolewa ili kama wanajipangia being kulingana na soko la dunia ijilikane.
Mtaalamu huyo wa masuala ya kilimo aliipongeza bejeti hiyo na kudai upande wa mifugo imetenda haki ,maabara kumi zinajengwa ,machinjio zinajengwa lakini isimamiwe kuwe na machinjio za kisasa na tuondokane na machinjio za kuchinjia chini kwa afya za binadamu .
Masawe pia alishauri ,soko la maziwa lipitie katika mashine ,kupimwa kwenye mitambo badala ya maziwa kutoka kwa mfugaji moja kwa moja kwenda kwa mlaji ili kulinda afya ya Mtanzania.