***************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba leo imeshindwa kufurukuta mbele ya maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa taifa ambapo wametoka sare ya mabao 1:1.
Simba ilianza kupata bao kupitia kwa winga wao machachari Shiza Kichuya mnamo dak.12 ya mchezo lakini bao hilo halikudumu sana kwani dk.37, Fully Maganga akaisawazishia klabu yake kwa bao safi la kichwa akimalizia krosi iliyopigwa kutokea pembeni ya uwanja.
Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kukaa kileleni mwa ligi Kuu Tanzania bara