Home Mchanganyiko MGUMBA AITAKA SEKTA YA KILIMO CHA UMWANGILIAJI NCHINI KUENDESHA MIRADI YAKE KIBIASHARA

MGUMBA AITAKA SEKTA YA KILIMO CHA UMWANGILIAJI NCHINI KUENDESHA MIRADI YAKE KIBIASHARA

0
Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akiwa na viongozi wa Tume ya Taifa ya umwagilijai akikagua magari pamoja na matrekta yanayotumiwa katika shughuli za kilimo mara baada ya kutembelea pamoja na kuzungumza na viongozi pamoja na wafanyakazi wa tume hiyo.
  
Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji nchini Bw.Daudi Kaali,akitoa taarifa za tume ya umwangiliaji kwa Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba ambaye alifanya ziara ya kuzungumza na vingozi pamoja na wafanyakazi  wa tume hiyo jijini Dodoma.

Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akizungumza na viongozi pamoja na wafanyakazi wa tume ya umwangiliaji jijini Dodoma.
Sehemu ya wafanyakazi wakimsikiliza Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na viongozi pamoja na wafanyakazi wa tume hiyo jijini Dodoma.
Baadhi ya matrekta yanayotumiwa na Tume ya umwangiliaji katika shughuli za kilimo.
Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi  wa Tume ya Taifa ya umwagilijai mara baada ya kuzungumza nao.

………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna, Dodoma
Serikali imeitaka sekta ya kilimo cha umwagiliaji nchini kuhakikisha  miradi yote ya umwagiliaji nchini  inaendeshwe kibiashara ili kurudisha mitaji na kupanua eneo la uwekezaji.
 Kauli hiyo imetolewa na Naibu  waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba, jijini Dodoma, wakati akizungumza na viongozi pamoja na wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya umwagilijai nchini (NIRC).
 Mhe.Mgumba amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne serikali imewekeza kiasi cha Sh. bilioni 96, katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji nchini lakini hakuna mapato ambayo serikali inayapa kutokana na miradi hiyo.
“Hivyo ni wakati sasa miradi yote ya umwagiliaji nchini, kuanza kuendeshwa kibiashara ili kurudisha mitaji mikubwa iliyowekezwa na serikali na kupanua eneo la uwekezaji huo katika sekta hiyo nchini”, ameeleza Mhe. Mgumba.
Aidha Mhe.Mgumba amesisitiza kuwa miradi ya umwagiliaji ndiyo ambayo imebakia kuwa sehemu ya serikali kuwekeza fedha bila kupata mapato hivyo sasa ni lazima tume ya Taifa ya umwagiliaji kuona namna ya kuendesha miradi hiyo kibiashara.
“Miradi hii inatumia fedha nyingi sana za uwekezaji kutoka serikali kuliko miradi mingine, lakini hakuna kiasi chochote ambacho serikali inakipata kwa hivi sasa, ukiangalia hata kwenye miraddi ya vituo vya afya pamoja na kuwa ni ya jamii lakini watu wanachingia, kumuona daktali tuu ni Sh. 8,000 au 10,000”amebainisha Mhe.Mgumba
Vilevile Mhe. Mgumba amesema kuwa bila miradi hiyo kuendeshwa kibiashara mtiririko wa ukuaji wa sekta hiyo utayumba kwani wawekezaji watakimbilia kwenye miradi inayo rudisha faida.
“Kama mradi tumewekeza bilioni tatu, tukipata faidi basi tutakwenda kuwekeza katika maeneo mengine ili kuwa na kilimo cha uhakika ambacho hakitegemeo maji ya mvua kwa asilimia 100, na kuongeza uchumi wetu, kuongeza pato la taifa pampja na kuwa na uhakika wa chakula ili kumpiga adui umaskini”ameongezea Mhe.Mgumba
Mhe. Mgumba amesisitiza kuwa ni lazima miradi yote ya umwagilijai ambayo serikali imewekeza kukusanya mapato angalau kwa asilimia tano ya mapato kwani mpaka sasa hakuna kilicho kusanywa.
“Ukizingatia miradi hii ni ya kiuchumi lazima tukusanye kitu, kwani hata miradi ile ambayo ni ya kijamii kama hospitali, barabara inatushinda katika uchangiaji wa mapato ya serikali hivyo ndugu zangu wa tume lazima tubadilike lazima tupate mwongozo haraka utakao tuweza kuyafanya haya”ameweka wazi Mhe. Mgumba.
Mgumba amesema kabla ya mwezi Julai mwaka huu, lazima kuwe na mfuko wa umwagiliaji pamoja na mwongozo wake utakao saidia katika uboresha sekta hiyo nchini.
Naye Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji nchini Daudi Kaali, amesema kuwa hali ya kilimo cha umwagiliaji nchini, Tanzania ina hekta milioni 29.4 zinazofaa kwa kilimo hicho.
“Kati ya hekta hizo, hekta milioni 2.3 zina uwezekano mkubwa wa kumwagiliwa, hekta milioni 4.8 zinauwezekano wa kati na hetka milioni 22.3 zinauwezekano mdogo wa kumwagiliwa”ameeleza Kaali.
Kaali amesema kuwa  kufikia mwaka 2015, kabla ya kuanza kwa tume ya umwagiliaji jumla ya hekta 461,000 zilikuwa zimeendelezwa kwa kilimo cha umwagiliaji.