Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na uwezeshaji wa upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria, kupitia wasaidizi wa kisheria nchini, Legal Services Facility (LSF), ambalo linakuza na kulinda haki za binadamu hasa kwa wanawake maskini and makundi mengine yaliyo katika mazingira hatarishi kwa kutoa ufadhili wa fedha kwa taasisi zinazotoa huduma za kisheria Tanzania, imefanya tathmini na kutoa ripoti ya upatikanaji wa haki za kisheria iliyotekelezwa tangu mwaka 2016.
Ripoti hii inatoa tathmini ya awamu ya pili ya programu ya miaka mitano inayofadhiliwa na shirika la Maendeleo la Denmark (DANIDA), Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) kupitia mfuko wao wa Maendeleo.
Katika ripoti hii ya kipindi cha kati cha utekelezaji wa programu hii kinachoishia Juni 2019 yaani miaka miwili na nusu ya utekelezaji, inaonyesha kwa kina sana utekelezaji wa programu hii katika awamu ya pili.
Akiongea katika taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya LSF Lulu Ngw’anakilala alisema kuwa “Progamu ya utekelezaji wa upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria imekuwa na mafanikio makubwa sana katika kuunganisha utamaduni ya kutafuta kurekebisha masuala ya kisheria katika jamii hasa kwenye masuala ya kisheria na haki za binadamu.
Aliongeza kusema kuwa kuna makubaliano muhimu na wadau kuwa msaada wa kisheria imeboreka sana tangu kuanza kwa utekelezaji wa programu hii na kuwa mikoa yote iliyotembelewa kuna mfumo wa huduma za msaada wa kisheria na katika kila wilaya iliyotembelewa kuna wasaidizi wa kisheria wanaofanyakazi kwa jitihada kubwa.
Kiini cha programu ni kutaka kujibu agenda ya kitaifa iliyopo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aliongeza kusema kuwa programu hii inaendana na mfumo wa kitaifa kama vile sharia ya Msaada wa Kisheria ya 2017, Mpango wa Taifa wa kumaliza unyanyasaji dhidi ya wanawake na Watoto wa 2017/18-2021/22 na sera ya masuala ya jinsia.
Programu hii pia inashughulikia Maendeleo endelevu katika ukamilifu wake.
Taasisi ya LSF inathamini uhusiano uliopo na serikali kupitia wizara kama vile TAMISEMI, Wizara ya Afya, Wizara ya Sheria kwa Tanzania bara na visiwani.
“Jukumu letu ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuweka mazingira ya upatikanaji wa haki na sharia kama kichocheo muhimu cha maendeleoa nchini. Wadau wetu katika utekelezaji huu wamekubali kuwa kuna uhusiano mzuri na ushirikiano kati ya watendaji serikali katika kiwango cha mikoa na katika halmashauri,” alisema Ngwanakilala.
Akiongea kuhusu ukusanyaji wa takwimu juu ya upatikana wa haki, Meneja wa Ufuatiliaji, Matokeo and Tathmini Said Chitung alisema kuwa miongozo ya mahojiano ilitengenezwa kwa kategori maalumu kutoka katika kiwango cha chini kabisa cha jamii.
Watoa habari kutoka katika jamii ya chini katika walichaguliwa kimkakati kutoka katika kata kwenye wilaya kwenye mikoa 28 ya Tanzania bara na visiwani ambapo watoa habari 287 walihojiwa.
Chitung aliongeza kusema kuwa wilaya mbili zilizochaguliwa katika mkoa ilikuwa moja katika makao makuu ya wiliya na nyingine katika wilaya iliyopo vijijini. Katika kila wilaya zilizochaguliwa kulitumika sampuli za kitaalamu ili kubainisha kata moja ambayo kuna uwepo wa shirika la LSF.
Programu ya upatikanaji wa haki inayofadhiliwa na LSF inalengo la kuwawezesha jamii kujua, kutumia na kutoa mwelekeo wa kisheria kupitia elimu ya kisheria na huduma za kisheria.
Programu hii imeimarisha mifumo wa kisheria kupitia uwezeshaji wa watoaji wa msaada wa kisheria kama vile wasaidizi wa kisheria inayosaidia kushughulikia masuala ya kisheria, haki za binadamu na kuwapa ujuzi ili kuweza kuanzisha kazi zinazowaingizia kipato.
Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya LSF Lulu Ngwanakilala (kati kati) akionyesha bango baada ya kuzindua kutoa ripoti ya upatikanaji wa haki za kisheria iliyotekelezwa tangu mwaka 2016 jijini Dar es Salaam leo. Shirika lisilo la kiserikali linalotoa huduma za kisheria nchini Legal Services Facility (LSF), ambalo linakuza na kulinda haki za binadamu hasa kwa wanawake maskini and makundi mengine yaliyo katika mazingira hatarishi kwa kutoa ufadhili wa fedha kwa taasisi zinazotoa huduma za kisheria Tanzania.
—