Home Siasa SIMBACHAWENE ATAKA URASIMU WA WATAALAMU USIDHOOFISHE JUHUDI ZA SERIKALI

SIMBACHAWENE ATAKA URASIMU WA WATAALAMU USIDHOOFISHE JUHUDI ZA SERIKALI

0

************************************

Na  Mohammed Mhina, Mpwapwa

Wataalam wa masuala ya fedha kwenye Halmashauri za Wilaya hapa nchini,  wmetakiwa kuacha urasimu wakati wa kufanya  maamuzi ya matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali katika kutekeleza miradi  ya maendeleo iliyokusudiwa.

Agizo hilo limetolewa  na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. George Simbachawene, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ya jimbo la Kibakwe kwa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dododma.

Akikabidhi kitabu hicho chenye kurasa 34 kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpwapwa Ndugu George Chigwiye, Mh. Simbachawene amesema kuwa baadhi ya watendaji kwenye halmashauri za wilaya wamekuwa wakichelewesha michakato ya utoaji wa fedha hizo na hivyo kusababisha ucheleweshwaji wa miradi ya huduma kwa wananchi.

 Mh. Simbachawene pia amesema kwa upande wake, ametekeleza kwa mujibu wa ahadi alizo ahidi kwa mwaka  2015 ametekeleza ilani hiyo kwa  zaidi ya asilimia 100% katika sekta ya afya ,elimu,miundo mbinu ,nishati na  huduma za jamii.

Alisema pamoja na kutekeleza ilani hiyo lakini pia anakerwa  na urasimu unaofanywa na watendaji wa  halmasahauri ambao wamekuwa wakisuasua  katika kuidhinisha   malipo  kwenda kutekeleza  miradi  ya maendeleo kupitia fedha za mfuko wa jimbo ambazo kimsingi zinakabidhiwa kwa halamashauri kwa ajili ya  utekelezaji wa miradi mbalimbali.

“Mfano fedha za kituo cha afya  Pwaga  nilizotoa kutoka mfuko wa jimbo kutengeza fenicha za kituo cha hicho tangu septemba mwaka 2019  lakini zilikuwa hazikutolewa  kwa  kwa wakati  huku watalaamu wakidai  watumie mfumo wa ushindani kwa makandrasi.” amesema Simbachewene.

Kwa mujibu wa kitabu chake cha  utekelezaji wa ilani  ya CCM kwa mwaka 2015 -2020 Simbachawene alisema kupitia  serikali ya awamu ya tano waliweza kuchonga barabara ambazo tangu  uhuru viiji hivyo havijawahi kuwa  na  barabara zinazopitika kwa nyakati zote.

Kwa uapnde wa elimu Mhe Simbachawene  alisema, miodombinu ya majengo ya shule za mingi   na sekondari yameboreshwa yakiwemo mabweni na vyumba vya madarasa.

Alisema  kwa muda mrefu Jimbo la Kibakwe  lenye  tarafa mbili kata 18 na vijiji 68 na vitongoji 322 lilikunyuma   katika upatikanaji wa hudama za jamii kama miundo mbinu ya barabara ,umeme  maji zahati na vituo vya afya.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa CCM wilayani Mpwapwa George Chigwiye alisema alisema taarifa ya utekelezaji wa ilani hiyo  utawasaidia kutadhimini kazi alizo zifanya  Mbunge wa jimbo la Kibakwe  katika kukisaidia chama  na kupunguza chanagamoto za maendeleo katika jimbo lake la kibakwe.

Naye  Katibu wa CCM wilayani Mpwapwa Jackson Shalluah, amesema  kama msimamizi wa Ilani katika wilaya ya Mpwapwa ameridhishwa kwa kiasi kikubwa na  utekelezaji  wa ilani  katika jimbo la kibakwe na hivyo kupelekea  Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuaminiwa  na wananchi .