************************************
Wataalam wa masuala ya fedha kwenye Halmashauri za Wilaya hapa nchini, wmetakiwa kuacha urasimu wakati wa kufanya maamuzi ya matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo iliyokusudiwa.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. George Simbachawene, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ya jimbo la Kibakwe kwa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dododma.
Akikabidhi kitabu hicho chenye kurasa 34 kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpwapwa Ndugu George Chigwiye, Mh. Simbachawene amesema kuwa baadhi ya watendaji kwenye halmashauri za wilaya wamekuwa wakichelewesha michakato ya utoaji wa fedha hizo na hivyo kusababisha ucheleweshwaji wa miradi ya huduma kwa wananchi.
Mh. Simbachawene pia amesema kwa upande wake, ametekeleza kwa mujibu wa ahadi alizo ahidi kwa mwaka 2015 ametekeleza ilani hiyo kwa zaidi ya asilimia 100% katika sekta ya afya ,elimu,miundo mbinu ,nishati na huduma za jamii.
Alisema pamoja na kutekeleza ilani hiyo lakini pia anakerwa na urasimu unaofanywa na watendaji wa halmasahauri ambao wamekuwa wakisuasua katika kuidhinisha malipo kwenda kutekeleza miradi ya maendeleo kupitia fedha za mfuko wa jimbo ambazo kimsingi zinakabidhiwa kwa halamashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
“Mfano fedha za kituo cha afya Pwaga nilizotoa kutoka mfuko wa jimbo kutengeza fenicha za kituo cha hicho tangu septemba mwaka 2019 lakini zilikuwa hazikutolewa kwa kwa wakati huku watalaamu wakidai watumie mfumo wa ushindani kwa makandrasi.” amesema Simbachewene.
Kwa mujibu wa kitabu chake cha utekelezaji wa ilani ya CCM kwa mwaka 2015 -2020 Simbachawene alisema kupitia serikali ya awamu ya tano waliweza kuchonga barabara ambazo tangu uhuru viiji hivyo havijawahi kuwa na barabara zinazopitika kwa nyakati zote.
Kwa uapnde wa elimu Mhe Simbachawene alisema, miodombinu ya majengo ya shule za mingi na sekondari yameboreshwa yakiwemo mabweni na vyumba vya madarasa.
Alisema kwa muda mrefu Jimbo la Kibakwe lenye tarafa mbili kata 18 na vijiji 68 na vitongoji 322 lilikunyuma katika upatikanaji wa hudama za jamii kama miundo mbinu ya barabara ,umeme maji zahati na vituo vya afya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilayani Mpwapwa George Chigwiye alisema alisema taarifa ya utekelezaji wa ilani hiyo utawasaidia kutadhimini kazi alizo zifanya Mbunge wa jimbo la Kibakwe katika kukisaidia chama na kupunguza chanagamoto za maendeleo katika jimbo lake la kibakwe.
Naye Katibu wa CCM wilayani Mpwapwa Jackson Shalluah, amesema kama msimamizi wa Ilani katika wilaya ya Mpwapwa ameridhishwa kwa kiasi kikubwa na utekelezaji wa ilani katika jimbo la kibakwe na hivyo kupelekea Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuaminiwa na wananchi .