Wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani kwa Tanzania Bara na Visiwani na Viti Maalum watachukua fomu kuanzia Julai 14 hadi 17, na mwisho wa kurudisha fomu ni Julai 17, 2020, saa 10 jioni.
Ratiba ya kumpata mgombea nafasi ya Rais inaanza Juni 15-30, 2020 ambapo itakuwa nafasi ya kuchukua fomu, kutafuta wadhamini na kurejesha.
Ameyasema hayo leo Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Mhe.Humphrey Polepole ambapo amesema kanuni za kupata wagombea ndani ya Chama kuanzia diwani mpaka rais ni wazi zinaonesha hakuna kama CCM.
“Tunataka viongozi ambao wanaufahamu mwendokasi wa Rais Magufuli na wanaochukia rushwa pamoja na kujua Yale yote yanayomnyima usingizi kiongozi wetu Mkuu wa Chama, lkn pia tunataka watu ambao wanaojua kwamba Tanzania tumechelewa”. Amesema Mhe.Polepole.
Aidha Mhe.Polepole amesema wanawaanzishia mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM, wagombea wa CCM wawe wanyeyekevu , kiwango chao cha nidhamu kiwe juu muda wote, wajishushe wasijipeleke mbele, chama kitaketi na kuamua huyu ni bora na anafaa. – @hpolepole,
Mhe.Polepole amemalizia na kusema kwamba hivi karibuni walikuwa na kikao na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nia yao ni kuhakikisha rushwa haipati nafasi katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho, wamefunga mitambo ya kudhibiti wavurugaji.