Home Biashara AHMED SALIM AISIFU BAJETI YA SERIKALI 2020/21 KWENYE KILIMO

AHMED SALIM AISIFU BAJETI YA SERIKALI 2020/21 KWENYE KILIMO

0

Mkurugenzi uzalishaji wa kampuni ya Asas Ahmed Salim 
*****************************

NA DENIS MLOWE, IRINGA

 

MKURUNGEZI wa Uzalishaji wa Kampuni ya Asas, Ahmed Salim  amesema ameisifu bajeti ya serikali iliyosomwa jana ya 2020/21 kuwa imeweka mfumo wa maendeleo ya viwandani na kupunguza umaskini kupitia kukuza sekta ya kilimo ambayo inaajiri zaidi jamii ya Watanzania.

 

Akipongeza bajeti hiyo iliyosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango wakati akizungumza na mwanahabari hizi, Ahmed Salim  aliisifu na kuipongeza serikali kwa kuwakumbuka zaidi tabaka la chini wanaotegemea kilimo kwa asilimia kubwa.

 

Alisema kuwa bajeti hiyo imewekeza fedha nyingi katika sekta muhimu za kijamii na kiuchumi zikiwamo za kilimo, miundombinu hali iliyosababisha kwa kipindi cha miaka minne sekta ya mifugo imefanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya bilioni 22 kutoka benki ya maendeleo ya kilimo ukilinganisha na mwaka 2015 ambapo hapakuwa na mkopo.


“Kwa Mujibu wa Bajeti ya jana kilimo ni Sekta kubwa na muhimu kwa maendeleo kutokana na mchango wake katika uchumi baada ya kuisoma nimeona kwamba katika mwaka 2017, sekta hiyo ilitoa ajira kwa Watanzania kwa asilimia 65.5, ikichangia asilimia 28.7 ya Pato la Taifa ambapo sekta ndogo ya mazao ilichangia asilimia 16.58” na kuongeza kuwa

 

“ Sekta ya Kilimo inachangia asilimia 65 ya malighafi za viwanda. Takwimu zinaonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2018, ukuaji wa Sekta ya Kilimo ulifikia asilimia 7.1. Ukuaji huu ulichangiwa na hali nzuri ya hewa na jitihada za Serikali za kuhakikisha kuwa pembejeo zinawafikia wakulima kwa wakati pamoja na uboreshaji wa miundombinu katika maeneo ya uzalishaji. 3.1 Upatikanaji” alisema Ahmed

 

 

Alisema kuwa anaunga mkono juhudi za serikali katika kujinasua na athari za mtikisiko wa kiuchumi duniani uliosababishwa na janga la dunia la ugonjwa wa Covid 19 hivyo  kwa kuongeza bajeti katika sekta ya kilimo utawezesha uzalishaji wa chakula cha ziada na kuimarisha miundombinu na mawasiliano ili kuweza kuhimili ushindani wa soko la kikanda na kidunia.

 

Alisema, serikali za magharibi zilibaini athari za mitikisiko huo mapema na kuanza kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na hali hiyo katika sekta za uchumi na fedha hivyo kitendo cha bajeti kuwakumbuka wakulima na viwanda itasaidia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya ndani ya nchi na kuwafanya wananchi kukuza kipato kupitia sekta ya kilimo.

 

Alisema kuwa dhima ya serikali ya kutoa huduma bora za kilimo, kuandaa mazingira bora kwa Wadau wa Kilimo, kuimarisha mfumo wa majadiliano ya Kisera, kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuiwezesha Sekta Binafsi kuchangia kikamilifu katika kilimo endelevu chenye tija, masoko ya uhakika na ongezeko la thamani ya mazao itasaidia kwa kiasi kubwa kukuza kipato cha Mtanzania.

 

Akisoma jana bajeti hiyo, Dk. Philipo Mpango alisema jana kuwa Serikali imepanga kubadilisha kilimo kutoka kuwa cha kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara.

 

Alisema kuwa Mabadiliko hayo yanafanyika kwa kuzingatia malengo ya kitaifa yaliyowekwa hususan nchi yetu kufikia kipato cha kati kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na kuongeza kuwa ni mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo unaoweka mkazo kwenye mapinduzi ya viwanda unaitambua Sekta ya Kilimo kama mhimili imara utakaowezesha upatikanaji wa malighafi za viwanda.

 

Aidha alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa Sekta Binafsi kwenye kuongeza mitaji, teknolojia na ubunifu, sekta hiyo inashirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wa hiyo utazingatia mazao ya kipaumbele kulingana na ikolojia za kilimo.

 

Dk Mpango alisema kuwa mazao yaliyopewa kipaumbele ni korosho, pamba, tumbaku, kahawa, chai, miwa, mahindi na mpunga. Mazao mengine, mikunde, viazi mviringo na vitamu, mazao ya bustani na mbegu za mafuta (alizeti, ufuta na michikichi).

 

Hivyo alisema kuwa mkazo umewekwa kuhakikisha kwamba pembejeo na zana za kilimo bora zinapatikana kwa kuimarisha utafiti, huduma za ugani na mafunzo upatikanaji wa masoko ya mazao na miundombinu ya uzalishaji.