Dodoma, Mei 29, 2026

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Khatibu M. Kazungu anautaarifu Umma  kuwa, Mkoa unatarajia kuanza mbio za Mwenge wa Uhuru tarehe 31/05/2026, ambapo utapokelewa rasmi katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mtera,Wilaya ya Mpwapwa, kabla ya kuanza mbio zake katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma. Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Wilaya zote 7 na Halmashauri 8 za Mkoa huu, kwa umbali wa kilomita 1,595.3 huku miradi 54 ya maendeleo ikipitiwa, ambapo miradi 21 itawekewa mawe ya msingi, miradi 2 itafunguliwa rasmi, miradi 20 itazinduliwa, na miradi 11 itakaguliwa. Miradi hiyo yote ina thamani ya shilingi 23,243,056,418.58 ambapo vyanzo vya fedha hizo ni; Serikali Kuu shilingi 10,605,347,151.67, mapato ya ndani ya Halmashauri  shilingi 4,103,038,865.71, michango ya Wananchi shilingi 1,841,600,000.00 pamoja na

Wafadhili na Wadau waliotoa shilingi 6,693,070,401.20. Ratiba ya mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Dodoma 2026 ni kama ifuatavyo

31/05/2026 – Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

01/06/2026 – Halmashauri ya Jiji la Dodoma

02/06/2026 – Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

03/06/2026 – Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

04/06/2026 – Halmashauri ya Mji Kondoa

05/06/2026 – Halmashauri ya Wilaya ya Chemba 2

06/06/2026 – Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

07/06/2026 – Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa

Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 ni: “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo.” Uongozi wa Mkoa wa Dodoma unatoa wito kwa Wanadodoma wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi na shughuli zote za Mwenge wa Uhuru ili kuienzi Tunu hii adhimu.

Tukikumbuka kuwa Mwenge wa Uhuru ni alama ya uzalendo,mshikamano, maendeleo na matumaini ya Taifa letu.