Afisa masoko kutoka TAMWA-ZNZ Muhidini Ramadhani akigawa mbegu za mchicha na pilipili kwa wajasiriamali kutoka Shehia ya Kiboje Unguja kwa lengo la kuwawezesha wajasirimali hao kiuchumi.
Afisa masoko kutoka TAMWA-ZNZ Muhidini Ramadhani akiwasomea mkataba wa makabidhiano ya vifaa wajasiriamali wa shehia ya Mtende Makunduchi mkoa wa kusini Unguja kabla ya kuwakabidhi rasmi vifaa mbali mbali ambavyo vitatumika kwa ajili ya uzalishaji mali.
Afisa Masoko kutoka TAMWA-ZNZ Muhidini Ramadhani akisisitiza jambo wakati alipokua akizungumza na wajasiriamali wa Shehia ya Kidutani Unguja mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vifaa mbali mbali.
***************************
Na Masanja Mabula , Zanzibar.
JUMLA ya Shilingi Milioni saba zimetumika na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-ZNZ kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbali mbali vya kuwawezesha wajasiriamali katika maeneo tofauti Unguja na Pemba huku lengo kuu likiwa ni kuwakuza wajasiriamali hao kiuchumi.
Msaada huo umekuja siku chache baada ya kufanyika kwa ziara ya Mkurugenzi wa Chama hicho Dkt,Mzuri Issa katika vikundi hivyo ili kujionea shughuli za uzalishaji pamoja na changamoto.
Akitoa taarifa kuhusu vifaa hivyo Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa alisema msaada huo umehusiaha vifaa tofauti kama vile vifaa vya kuwezesha wajasiriamali zao kutengeza sabuni pamoja na kuwawezesha katika shughuli za kilimo.
Alisema wiki moja iliopita baada ya kufanya ziara katika maeneo yote ambayo Chama hicho kinawezesha wajasiriamali hao walipata maombi ya wahusika na kuona ni vyema kuyafanyika kazi.
Alisema kwa kuwa zipo jitihada kubwa zinazoendelea kufanya wakaona ipo haja ya kuwaunga mkono ikiwemo pamoja na kuwapatia vifaa.
Akitoa ufafanuzi wa vikundi ambavyo vitafaidika na msaada huo kwa upande wa Unguja alisema ni vikundi 12 na kwa Pemba ni 24 vikundi ambavyo vyote vimeanzishwa miezi mitatu iliopita chini ya usimamizi wa TAMWA-ZNZ.
Awali afisa masoko kotoka TAMWA-ZNZ Muhidini Ramadhani aliwataka wajasiriamali hao kuwa makini sambamba na kuhakikisha utunzaji wa vifaa hivyo kwa muda wote.
Alieleza kuwa iwapo vifaa hivyo vitatumika ipasavyo vitaweza kuleta tija kubwa ikiwemo kusaidia maendeleo kwa wananchi hao na Taifa kwa ujumla.
Lakini pia Afisa huyo alieleza kuwa Zanzibar kwa sasa kuna fursa nyingi ikiwemo za matunda na mboga mboga hivyo kuna kila sababu wajasiriamali hao kuzitumia.
Kwa nyakati tofauti baadhi ya wanjasiriamali hao kutoka mkoa wa kusini Unguja walieleza kufuurahishwa kwao na hatua hio muhimu iliofanywa na TAMWA-ZNZ na kwamba wanaahidi vifa hivyo wataendelea kuvitunza ili viweze kuleta tija kwao.
Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mbegu za mboga mboga,keni za maji na trea zinazotumika kuzalisha sabuni