******************************
NJOMBE
Serikali mkoani Njombe imefanikiwa kuokoa zaidi ya bil 4 kati bil 7.9 ambazo zilikuwa hatarini kutafunwa na watu wachache ambao walikopa fedha katika vyama vya ushirika na benki ya wananchi Njombe NJOCOBA na kushindwa kurejeshwa mpaka pale serikali ilipoamua kuingilia kati.
Kwa mujibu wa taarifa za serikali zinasema kiasi cha bil 1.48 za Njocoba na zaidi ya bil 6.5 zilikopwa katika vyama vya ushirika na kutokomea nazo jambo ambalo likasababisha vyama vingi vya ushirika kufa na vingine kujiendesha kwa kusuasua.
Kitendo cha benki ya wananchi kufilisika kwasabau ya fedha nyingi kukaa muda mrefu kwa watu wachache huku baadhi ya vyama vya ushrika vikijiendesha kwa kusuasua kulimsukuma mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka mwishoni mwa mwaka jana kuanza kufatilia madeni hayo na kufanikiwa kupata kukusanya zaidi ya bil 4 ambazo zinawekewa utaratibu wa kurejesha kwa wananchi kwa utaratibu maalumu.
Ufafanuzi juu ya kiwango cha fedha kilichokusanywa na lini zitatolewa kwa wananchi waliokuwa wameweka fedha jocoba na vyama vya ushirika ulikuja baada ya mbunge wa jimbo la makambako Deo Sanga kuomba serikali kuanza kugawa fedha iliyopatikana ili kuwasaidia wanachama katika kipindi hiki kigumu.
Inje ya ukumbi wa mikutano baadhi ya madiwani akiwemo Imany Fute,Eda Nyagawa na Baraka Kivambe wakaeleza jinsi kufa kwa benki ya wananchi Njombe na vyama vya ushirika kulivyoathiri maisha ya wananchi wengi ambapo wamesema kuwa fedha hiyo ilikuwa ikitumika kuendesha maisha yao kwa kusomesha watoto,biashara na kilimo.