Home Mchanganyiko JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAMSHIKILIA DEREVA WA LORI MALI YA...

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAMSHIKILIA DEREVA WA LORI MALI YA TEXAS HARDWARE KWA KUSABABISHA AJALI ILIYOPELEKEA VIFO VYA WATU 8 NA MAJERUHI 5 WILAYA YA MAGU

0

***********************************

TAREHE 10.06.2020 MAJIRA YA  19:45HRS KATIKA BARABARA YA MWANZA – MUSOMA, ENEO LA IHAYABUYAGA, KATA YA BUKANDWE, TARAFA YA SANJO, WILAYA YA MAGU – MWANZA, DEREVA AITWAE BONIPHACE CLIPHORD @TUJU MIAKA 37, MJITA, MKAZI WA MWANZA-NERA AKIENDESHA GARI NA T.322 DCB TRAILER T.1351 DCA AINA YA SCANIA LIKITOKEA WILAYA YA BUSEGA KWENDA MWANZA MALI YA KAMPUNI YA TEXAS HARDWARE, ILIGONGA  TELA YA TRAKTA KWA NYUMA AMBAYO ILIKUWA HAINA TAA ZA NYUMA YENYE NAMBA ZA USAJILI T.952 DGW, BAADA YA KULIGONGA ILIHAMA NJIA NA KUGONGANA NA GARI ILIYOKUWA NA ABIRIA KUTOKA MWANZA KWENDA MAGU YENYE NAMBA ZA USAJILI T.775 DEG AINA YA NISSAN, INAYOMILIKIWA NA  GEORGE [email protected] AMBAYE ALIKUWA DEREVA WA GARI HIYO NA KUSABABISHA VIFO VYA ABIRIA 8 NA MAJERUHI WATANO ABIRIA  WALIO FARIKI NA MAJERUHI WOTE NI WANAUME.

MAREHEMU AMBAO WAMETAMBULIWA NI:-

  1. GEORGE MSANGI, MPARE, DEREVA WA HIACE MKAZI WA MAGU.
  2. HAMIS MASIGE, MIAKA 35, MJITA, MWALIMU LUHENGE SECONDARY, MKAZI WA LUGEYE.
  3. WALIOFARIKI WENGINE 6 BADO HAWAJATAMBULIKA, WOTE NI WANAUME.

MAJERUHI AMBAO WANAPATIWA MATIBABU BUGANDO HOSPITALI NI:-

  1. AYUBU MINDULE, MNYATURU, MRATIBU ELIMU KATA YA CHABULA, MKAZI WA NYANGUGE
  2. ELIAS LUTANDULA, MIAKA 46, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA NYANGUGE.
  3. KASABUKU KISHELA, MIAKA 32, MKULIMA, MSUKUMA, MKAZI WA MAGU.
  4. EDIBINI MAKUBO, MIAKA 20, MHAYA, MWANAFUNZI, KIDATO CHA SITA, BARIADI HIGH SCHOOL, MKAZI WA NYANGUGE.
  5. ELIAS FRANCIS, MIAKA 44, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA NYANGUGE, YEYE AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MAGU.

 

UCHUNGUZI KUHUSU AJALI HII UNAKAMILISHWA. MIILI YA MEREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO KWA UTAMBUZI NA UCHUNGUZI WA DAKTARI.

JESHI LA POLISI LINATOA WITO KWA MADEREVA WOTE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI NA KUCHUKUA  TAHADHARI KWA KUFUATA SHERIA NA  ALAMA ZA BARABARANI WAKATI WOTE  WANAPOTUMIA BARABARA.