Home Mchanganyiko SHULE ZINA UPUNGUFU WA MADARASA

SHULE ZINA UPUNGUFU WA MADARASA

0

Diwani wa kata ya Makanyagio Haidari Sumri akikabihi tofali kwa Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Matinga analosaidiwa kubeba na mtendaji wa Kashaulili

Matofali 3000 yaliyotolewa na diwani wa kata ya Makanyagio Haidari Sumri

……………………………………………………………….

Na. Zillipa Joseph,Katavi

Shule za msingi za Kashato na Katavi zilizopo katika kata ya Makanyagio manispaa ya Mpanda mkoani Katavi zinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 40 hali inayopelekea wanafunzi wa shule hizo kusoma wakiwa katika msongamano mkubwa

Akitoa taarifa ya shule hizo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa; mtendaji wa kata ya Makanyagio bwa na Mussa Athumani amesema shule hizo zina jumla ya wanafunzi 2741

Aidha bwana Athumani ameeleza kuwa wana upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Matinga amewashukuru wadau mbalimbali wa maendeleo kwa kuchangia ujenzi huo

Katika harambee hiyo iliyoitishwa na diwani wa kata ya Makanyagio Haidari Sumri ambaye amechangia matofali 3000 ya bloku; fedha taslimu shilingi milioni 2.4 zilipatikana pamoja na michango mbalimbali ya saruji na vifaa vingine vya ujenzi

Sumri ambaye pia mwaka 2018 alichangia matofali 10,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ameshukuru kwa mahusiano mazuri waliyonayo viongozi mbalimbali wa serikali, na wa siasa katika kata hiyo hali inayopelekea kutatua changamoto za wananchi kwa pamoja