Home Mchanganyiko MNEC HAJI JUMAA AMFAGILIA MAKONDA KWA KUPIGANIA KUNDI LA VIJANA

MNEC HAJI JUMAA AMFAGILIA MAKONDA KWA KUPIGANIA KUNDI LA VIJANA

0
…………………………………………………………………………..
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC Pwani ),Haji Jumaa amempa tano ,mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa kupigania kero mbalimbali ,ikiwemo hatua aliyochukua kukemea baadhi ya askari wa Jiji hilo kuacha kuwabugudhi waendesha bodaboda kwa kuelekeza mamlaka husika kuwaruhusu kuingia Mjini.
Hatua hiyo itawezesha kusaidia zaidi ya familia milioni moja  kwa wastani wa watu 10 kwa kila muendesha bodaboda, ,kwa idadi ya abiria wanaotumia bodaboda zaidi ya laki tano kwa siku.
Akizungumzia kuhusiana na ajira na kundi la vijana linavyostahili kupiganiwa ,ili kujiinua kimaisha, Haji alisema,huenda kazi anayoifanya Makonda isiwe inaonekana kutokana na watu kuangalia vitu vidogo visivyo na tija kwa vijana.
“;:Binafsi naweka wazi kutambua kazi inayofanywa na kijana mwenzetu Paul Makonda, kutokana na uongozi wake mahiri katika kutatua kero mbalimbali za Mkoa wa Dar es Salaam, mkoa ambao unaongoza kwa changamoto lakini amemudu kuzitatua kadiri alivyojaaliwa na Mungu.
” Ki ukweli huo ni uamuzi wa kiutu, utu unaongalia maslahi mapana ya uchumi wa Jiji na vijana kwa ujumla, ieleweka kwa sasa Dar es Salaam ina zaidi ya waendesha Bodaboda laki moja (100,000).”alifafanua Haji .
Haji alieleza, wengi hawakukifikiria; ni namna nzuri tunayoweza kuwatumia waendesha bodaboda katika kuwajumuisha kwenye kamati za ulinzi na usalama kupitia viongozi wao.
“Kofia zao ngumu zinaweza kutumika kufunga ‘Camera’ za ulinzi ili kurekodi matukio yanayoendelea mjini, inaweza kuwa wazo lenye tija na manufaa kwa jamii,hatuna sababu ya kuweka mbele maslahi binafsi, chuki na visasi havisadii kujenga viongozi vijana; 
” Sote tunafahamu ukubwa na umuhimu wa Jiji la Dar es Salaam, kitendo cha Rais Dk. John Magufuli kumteua kushika nafasi hiyo ni ishara kuwa ana imani naye, kinachotakiwa ni kumtia moyo na kumshauri kwa heshima, pale inapoonekana kakosea kwa kuwa hakuna mkamilifu chini ya jua.;”alisisitiza Haji.
Haji anabainisha kwamba, binafsi yake ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu wa Chama Taifa, anaona mkuu huyo wa mkoa amekitendea haki Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika siasa za Mkoa wa Dar es Salaam.
Makonda amekuwa kifua mbele kufuatilia miradi mbalimbali ya kitaifa na kimkoa, amekuwa akishughulika na makundi maalumu kama wajane, walemavu na wagonjwa.,na ameondoa kero za ofisi za walimu.