*******************************
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
WAFANYABIASHARA ndogondogo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani,wameanza rasmi kazi kwenye bandari ndogo wilayani hapa, baada ya kusimama kwa takribani miezi mitatu.
Hatua hiyo imetokana na Mkuu wa wilaya hiyo Zainab Kawawa kukaa nao pamoja na Maofisa wanaosimamia Bandari hiyo, kufanikiwa kumaliza tofauti hiyo, hatimae kuanza tena shughuli zao.
Akizunguma katika Bandari ndogo wilayani humo, Kawawa alisema kuwa kunyanyaswa kwa wafanyabiashara hao ni sawa na kumnyanyasa yeye, kwani wamekuwa wakichangia kupatikana mwa mapato zaidi ya shilingi bil. 2.5 hadi 3.
“Uwepo wa wafanyabiashara wakubwa wanaoagiza bidhaa mbalimbali zikowemo za mafuta, zinawasaidia hawa wadogowadogo ambao nao hutumia fursa hiyo kuagiza madumu ya mafuta kuanzia mawili na kuendelea, hivyo kuongeza upatikanaji wa mapato zaidi,” alisema Kawawa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bagamoyo,Abdul Sharifu, alimpongeza Kawawa kwa namna anavyotekeleza majukumu yake, na kwamba ameonesha namna gani Rais John Magufuli alivyofanya uteuzi sahihi uliolenga kupatikana kwa kiongozi anayejali shida za wana-Bagamoyo.
Akishukuru kwa niaba ya walimu wilayani hapa, Victoria Kesi Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi wa Nyaraka alitoa shukranu kwa Mkuu wa Wilaya kwa juhudi zake, huku akimpongeza Patel kwa namna anavyojitoa kwenye shughuli za kimaendeleo.