**************
03/06/2020 SENGEREMA MWANZA
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka wananchi kuendelea kuchukua hatua ikiwemo kujilinda dhidi ya majanga ya moto ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kwenye maeneo yao.
IGP Sirro amesema hayo leo akiwa Kisiwa cha Kome Mchangani wilayani Sengerema mkoani Mwanza, wakati akiongea na baadhi ya wananchi wa kisiwa hicho ambao mwezi Mei mwaka huu walikumbwa na ajali ya moto ulioteketeza mali zao.
Aidha, IGP Sirro ameendelea kuwataka wananchi kuendelea kuchukua hatua ikiwemo kuwafichua raia wa kigeni ambao ni wahamiaji haramu wanaoingia nchini bila kufuata utaratibu.