Home Siasa CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA VYAMA VITAKAVYOKUWA TAYARI KUSHIRIKIANA

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA VYAMA VITAKAVYOKUWA TAYARI KUSHIRIKIANA

0

********************************

Na Magreth Mbinga

Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA imefungua mlango kwa vyama vingine vya Siasa ambavyo vitakuwa tayari kushirikiana.

Amezungumza hayo habari Katibu Mkuu wa Chama hiko John Mnyika Makao Makuu ya Chama Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Aidha amewataka wanachama wa Chama hiko ambao wanania ya kugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwasilisha taarifa kwa Katibu mkuu na kujadiliwa na kamati kuu kwa mijibu wa Katiba ya Chama hiko.

Vilevile Mnyika amesema mlango huo wa kutia nia ya kugombea nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania umefunguliwa leo na utafungwa June 15 mwaka huu.

Sanjari na hayo Mnyika amesema zoezi hilo la kutia nia ya Urais ni mchakato wa ndani wa Chama amboa utafatiwa na hatua nyingine ambao utatangazwa hapo baadae.

Hata hivyo Mnyika amesema dhamira ya kufungua mlango huo wa kutia nia haujafunga majadiliano na vyama vingine .