Koplo Brown Twaibu akichapa mwendo kwenda kupokea pongezi ya fedha taslim TSHs 1,000,000 kutoka Benki ya NBC, TSHs 200,000 na cheti cha pongezi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Lazaro Mambosasa iliyowasilishwa na Kamanda Polisi wa Ilala, Kamishna Msaidizi Zuberi Chembera (wapili kushoto) katika hafla ndogo iliyofanyika katika kituo cha Polisi cha Salander Bridge. Wengine katika picha Mkuu wa Mawasiliano wa Benki ya NBC Nd. David Raymond.
Koplo Brown Twaibu akipokea mkono wa pongezi ya fedha taslimu milioni moja kutoka Bw. David Raymond Kigwire Mkuu wa mawasiliano wa Benki ya NBC kwa kuhamasisha jamii juu ya uvaaji wa barakoa kwa dhumuni la wananchi kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya Korona, katika hafla ndogo iliyofanyika katika kituo cha polisi cha Salender Bridge.
RPC wa Ilala Zuberi Chembera akimkabidhi Koplo Brown Twaibu cheti cha pongezi kwa kazi njema aliyoifanya ya kuelimisha jamii juu ya uvaaji wa barakoa kwa dhumuni la wananchi kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya Korona, katika hafla ndogo iliyofanyika katika kituo cha polisi cha Salender Bridge.
…………………………………………………………………………………………
Benki ya NBC leo imetambua juhudi mahususi za Jeshi la Polisi Tanzania na maofisa wake katika kipindi chote cha mlipuko wa homa kali inayosababishwa na virusi vya Covid-19 maarufu kama corona. Katika matukio mbali mbali ya kipekee, maofisa kwa Jeshi la Polisi Tanzania wameonyesha hekima ya hali ya juu na dhamira ya kuwatumikia, kuwalinda na kuhakikisha Watanzania wanatekeleza maelekezo ya wataalam ya jinsi ya kupambana na ugonjwa wa corona.
Aidha, benki hiyo ikishirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania pia imemtambua na kumpongeza Koplo Brown Twaibu Msoke kwa kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuvaa barakoa katika kupambana na gonjwa la corona. Koplo Taibu alijizolea umaarufu baada ya video ikimuonyesha akiwahimiza abiria kwenye daladala kufuata maelekezo ya serikali kama kuvaa barakoa, kutosimamisha abiria kwenye usafiri wa umma na kukaa umbali wa mita moja siyo kwa kujilinda tu bali kuwalinda na wengine.
Akiongea katika hafla hiyo, Mkuu wa Mawasiliano wa NBC Nd. David Raymond Kigwile alisema “Kufikia maamuzi ya kumpongeza Koplo Taibu ilikuwa kitu rahisi kwa benki yetu, hususan kwa sababu vitendo vyake vya kishujaa vinaendana na msimamo wa benki yetu katika kupambana na virusi vya Covid-19.” Itambulike kuwa Benki ya NBC pia imechukua hatua madhubuti kupamba na kuenea kwa virusi hivyo kama kuwa benki ya kwanza kuweka vitakasa mikono katika ATM zake zote nchini, utekelezaji wa nafasi ya mita mbili katika matawi yake. Benki ya NBC pia itaendelea kuwahamasisha na kuwaelimisha wafanyakazi wake na Watanzania kwa ujumla jinsi ya kumpambana kwa ugonjwa huyo.
Aidha RPC Ilala Nd. Zuberi Chembera alisema, “Koplo Twaibu ameonyesha mfano mzuri wa kuhamasisha jamii juu ya uvaaji wa barakoa kwa dhumuni la wananchi kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona. Kitendo hicho ni mfano wa kuiga na kinahitaji pongezi ya pekee hususan kipindi hiki ambacho dunia nzima inapambana na janga hili.
Pamoja Benki ya NBC kumtunuku Koplo Brown Msoke fedha taslim TSHs. 1,000,000 na kumfungulia akaunti katika benki hiyo, Jeshi la Polisi Tanzania pia limemzawadia Koplo Twaibu kiasi cha TSHs 200,000 na cheti maalumu kutoka kwa Kamanda wa Polizi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.
Katika kuendeleza dhamira ya kuelimisha jamii matumizi sahihi ya barakoa, Benki ya NBC imezindua kampeni yake mpya ya #NBCBarakoaChallenge. Pamoja kuhimiza uvaaji wa barakoa, kampeni ya #NBCBarakoaChallenge itakayoendeshwa kupitia mitandao ya kijamii ya NBC inaangalia pia kuwakumbusha na kuelimisha Watananzania juu ya umuhimu wa kuzingatia tabia kinga ili kuzuia Covid-19.
Jinsi ya kushiriki Barakoa Challenge
- Jipige picha ukiwa umevaa barakoa.
- Post kwenye ukurasa wako wa Instagram ukiwa na hashtag #NBCMaskChallenge.
- Watag watu watatu uwaandikie ujumbe wa kuwakumbusha kuvaa barakoa.
Post yenye likes nyingi zaidi kujishindia simu janja aina ya Samsung A10s kila wiki.
Hakikisha akaunti yako haiko private ili tuweze kuona post yako.
Vigezo namsharti kuzingatiwa
Kuhusu National Bank of Commerce (NBC)
Benki ya Taifa ya Biashara, NBC ni benki ya zamani kuliko zote nchini Tanzania ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitano. Tunatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wa rejareja, biashara, mashirika na misaada ya uwekezaji, bidhaa na huduma za usimamizi mzuri wa fedha.
Benki hii inaanzia mwaka 1967 ambapo Serikali ya Tanzania ilibinafsisha taasisi zote za fedha, zikiwamo benki. Mwaka 1991, sheria ya mabenki ilirekebishwa na miaka sita baadae, yaan mwaka 1997, taasisi iliyojulikana kama Benki ya Taifa ya biashara, iligawanywa ka;ka tanzu tatu tofau;: NBC Holding Corpora;on, Na;onal Microfiance Bank (NMB) na NBC (1997) Limited. Mwaka 2000, Benki ya Afrika Kusini, Absa Group Limited, ilipata hisa 55% kutoka NBC (1997) Limited. Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania ilipata 30% ya hisa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kama mwanachama wa Benki ya dunia (World Bank Group), ilipata 15% ya hisa za benki hii. Taasisi hiyo mpya ikaitwa NBC Limited.
Benki ya NBC ni benki pekee ya kimataifa inayopa;kana ka;ka maeneo mbalimbali nchini. Ikiwa na matawi 5 na mashine za ATM zaidi ya 230, Benki ya NBC inatoa huduma mbalimbali za ukusanyaji fedha za huduma nyingine za kibenki kwa wateja mbalimbali. Benki ya NBC sasa imeajiri wafanyakazi takriban 1,200 nchi nzima.
Kwa maelezo zaidi au msaada tupigie +255 76 898 4000/4011 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 or email us [email protected]