Home Mchanganyiko USHIRIKIANO UNAHITAJIKA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA HAKI ZA WATOTO

USHIRIKIANO UNAHITAJIKA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA HAKI ZA WATOTO

0

RIPOTI ZA WATOTO

Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt amewataka wadau mbalimbali wanaohusika mashauri na haki za watoto kushirikiana ili kuweza kutatua changamoto   zilizopo katika mahabusu   na baadhi ya magereza ili hakikisha mtoto anapatiwa haki kwa wakati na katika mazingira bora, ikiwemo kulindwa.

Akizungumza leo wakati akifungua kikao kazi cha wadau wa Mahakama baada ya kufanyika ukaguzi wa mahabusu za watoto na baadhi ya magereza ulifanyika kuanzia Machi 16 hadi Machi 25, mwaka huu kilichofanyika kwenye Kituo cha Habari cha Mahakama ya Tanzania (JMC, kilichopo Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

Alisema moja ya jukumu la Mahakama Kuu Masjala Kuu ni kukagua Mahakama zote za chini,magereza na mahabusu za watoto nchini ili kuboresha huduma za Mahakama kwa kuhakikisha haki inapatikana kwa wote na kwa wakati

Msajili huyo alisema kila mdau ana wajibu wa kufanikisha haki ya mtoto inapatikana kwa wakati, ikiwemo kutafuta suluhisho la changamoto zilizojitokeza katika ukaguzi huo kwa haraka.

 “Miongoni changamoto iliyojitokeza katika ukaguzi huo kuna baadhi ya watoto walikutwa katika gereza la watu wazima kwa sababu ya kushindwa kutathimini umri wao wakati wa kuaandaa hati zao za mashtaka na hivyo kusomeka ni watu wazima. Katika suala hili ni jukumu la kila mdau kuweza kuangalia jinsi ya kulitatua,” alisema Mhe. Sarwatt.

Kwa Naibu Msajili wa Mahakama wa Kuu ya Tanzania Dawati la Watoto, Mhe. Nyigulila Mwaseba alizitaja changamoto nyingine zilizopo katika ukaguzi huo, kuwa ni  watoto waliokinzana na sheria  kupigwa wakati wa kukamatwa hali inayowasababishia baadhi yao kupata ulemavu wa kuhudumu hasa katika mkoa wa Dare es Salaam,  kutokuwepo kwa mahabusu za watoto hali inyosababisha watoto kuchanganywa na watu wazima katika magereza.

Nyingine Maafisa Ustawi wa Jamii hawahusishwi katika hatua za ukamataji wa watoto ili haki zao za msingi zifuatwe, baadhi ya majengo ya mahabusu ni chakavu na yana maeneo finyu hivyo kuwanyima uhuru watoto na nafasi ya kujifunza kwa vitendo,ikiwemo kuwabadilisha tabia, upungufu wa Maafisa Ustawi wa Jamii, kutokuwepo kwa fungu la kuwahudumia watoto waliokutana na sheria magerezani( watoto waliopo gerezani baada ya mama zao kutumiwa na kosa la jinai au kufungwa) na kutokuwepo kwa usafiri katika mahabusu za watoto na kusababisha kutofikishwa mahakamani kwa wakati.

Akichangia hoja kuhusu kuwepo kwa bajeti au fungu la kuwahudumia watoto waliokutana na sheria magerezani (waliopo gerezani baada ya mamazao kutuhumiwa na kosa la jinai au kufungwa na kuwarekebisha watoto waliokinzana na sheria, ikiwemo kuwepo kwa mazingira wezeshi ya kusomea. Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Amina Kavirondo alisema kuna haja ya kupaza sauti ili bajeti kwa ajili hiyo itengwe kwa ajili hiyo.

Wadau hao, pia walipendekeza kuwepo kwa mikakati ya kuanzisha mahabusu za watoto waliokinzana na sheria.

Ukaguzi huo ulifanyika baada ya Jaji Kiongozi kuteua timu ya watu sita, ambayo ilifanya kazi hiyo kwenye mahabusu nne za watoto.zilizopo mikoa ya Dar es Salaaam, Tanga, Moshi, Arusha na Mbeya, Shule ya Maadilisho iliyopo Irambo – Mbeya na baadhi ya magereza ambayo ni gereza la Maweni, Karanga, Ruanda, Kisongo, Chumbageni.

Jumla vituo 13 na watoto 131 walihusika katika ukaguzi huo,