Home Mchanganyiko SANAA INAGUSA SEKTA ZOTE MUHIMU

SANAA INAGUSA SEKTA ZOTE MUHIMU

0

**********************************

Na Magreth Mbinga

Mkurugenzi mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania BASATA Bw.Godfrey Mngereza amesema Sanaa ni pana sana inagusa sekta zote muhimu za Binadamu.

Amezungumza hayo leo katika mkutato wa Bodi ya Sanaa uliofanyika katika ukumbi wa BASATA ambapo ulishirikisha wadau mbalimbali ambao ni wadau wa Benki,Shirikisho la Sanaa Afrika,Shirikisho la Ufundi,Shirikisho la Muziki na Wadau wengine mbalimbali katika kujenga sekta ya Sanaa hususa katika kipindi hiki cha Corona.

Pia Rais wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw.Michael Sangu amesema shirikisho la Filamu ilichukua hatua ya kusimamisha kazi za Filamu wakati ugonjwa wa Corona uliposhamili.

Vilevile Bw.Sangu amesema kuwa mabo ambayo watayatazama wakati wa utengenezaji wa Filamu ni kuwa na watu wachache wakiwa wanaandaa Filamu husika ili kujikinga na maambikizi ya Corona.

Sanjari na hayo Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho amesema Bw.William Chitanda amesema sherehe ziruhusiwe lakini tahadhari zichukuliwe kwenye ukumbi kuwe na kipima joto na vitakasa mikono pia wakati wa kutoa zawadi sio lazima washikane mikono.

“Ukumbi uwe mkubwa ambao utazingatia watu kuto kukaribiana hata wakati wa kupata chakula na wakati wa kucheza Muziki watu wavae barakoa”amesema Bw.Chitanda.

Hatahivyo Meneja wa bendi ya Msondo Ngoma Said Kiberiti amezungumza kwa niaba ya wamiliki wa bendi Tanzania amewataka wasanii kufata miongozo ya Serikali hivyo wasijichanganye wenyewe kwakuwa kila mmoja anajua mazingira ya kazi yake.

“Ni vema wanamuziki tutoe changamoto ambazo tunakutana nazo katika mazingira ya kazi zetu ili kuishawishi Serikali itusaidie katika shughuli zetu”amesema Kiberiti.