Home Mchanganyiko KAMPUNI YA VODACOM TANZANIA YAKABIDHI VIFAA VYA SH 42 MILIONI KITUO CHA...

KAMPUNI YA VODACOM TANZANIA YAKABIDHI VIFAA VYA SH 42 MILIONI KITUO CHA AFYA MURIET

0
Meneja wa kampuni ya Simu za mkononi Vodacom Tanzania Kanda ya kaskazini, George Venanty akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo vifaa walivyokabithi katika kituo Cha afya cha Muriet.
Meneja wa kampuni ya Vodacom Tanzania ,Kanda ya kaskazini George Venanty akizungumza katika hafla ya kukabithi vifaa hivyo vyenye thamani ya shs  42 milioni kwa kituo Cha afya Muriet kilichopo mjini hapa.
Aliyeko kushoto mwenye tisheti nyekundu ni Meneja wa kampuni ya Vodacom Tanzania Kanda ya kaskazini , George Venanty akimkabithi Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo baadhi ya vifaa hivyo kwa ajili ya kituo Cha afya cha Muriet kilichopo jijini Arusha.
Picha Na.Happy Lazaro
……………………………………………………………………..
Happy Lazaro,Arusha.
Kampuni ya Vodacom Tanzania  imekabithi vifaa vya shs 42  milioni kwa kituo Cha afya  cha Muriet kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya siku (njiti).
Aidha akipokea  msaada huo kutoka kampuni ya Vodacom ,Mkuu wa Mkoa wa  Arusha ,Mrisho Gambo amewataka wananchi wa kata ya Muriet  hasa wanawake mkoani Arusha kutumia ipasavyo uwepo  wa  vifaa hivyo  vipya vya kisasa vilivyotolewa na kampuni hiyo ili kuweza kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.
Gambo ameyasema hayo jijini Arusha wakati akipokea msaada wa vifaa hivyo vya  kuhudumia watoto njiti wanaozaliwa katika kituo hicho Cha afya cha Muriet mkoani Arusha.
Gambo alisema kuwa, Ni vizuri wananchi wakatumia ipasavyo kituo hicho kwani kwa Sasa hivi kinafanya kazi masaa 24 lengo likiwa Ni kuhakikisha wananchi wote wanahudumiwa kwa wakati .
Amesema  kuwa,uwepo wa vifaa hivyo itasaidia Sana kuondoa changamoto iliyokuwepo ya watoto waliokuwa wakizaliwa njiti ambapo ilikuwa ikiwalazimu kwenda kupata huduma  katika hospital za mjini.
Aidha alisema kuwa,wapo katika harakati za kutafuta gari nyingine kubwa ya kubebea wagonjwa kutokana na kuwa iliyopo Ni ndogo kulingana na ukubwa wa kituo hicho.
Meneja wa  kampuni  ya Vodacom Kanda ya kaskazini ,George Venanty alisema kuwa,wamekuwa wakijiwekea mikakati mbalimbali ya kusaidia jamii kwa kuchangia vifaa mbalimbali vya tiba.
Venanty alisema kuwa,wamekabithi vifaa hivyo venye thamani ya shs 42 milioni ambapo vifaaa hivyo Ni kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati(njiti)lengo likiwa Ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki iliyo Bora na kwa wakati.
Naye Diwani wa kata ya Muriet ,Francis Mbise alisema kuwa,wanashukuru kwa kuletrwa kituo hicho kwani kimeweza kurahisisha huduma za afya kwa wananchi hao kwani walikuwa wakifuata huduma hizo mjini na kwa Sasa hivi huduma inapatikana masaa 24.
Mbise alisema pamoja na mafanikio mbalimbali Bado wanakabiliwa na changamoto ya uzio kwa ajili ya  kituo hicho kwa ajili ya usalama wa watumishi hao.
Mbise alisema kuwa,anaishukuru serikali kwa kuwekeza katika kituo hicho ambacho hivi Sasa wameweza kutoa huduma mbalimbali kwa muda wa usiku na mchana na kuweza kurahisisha changamoto ya kufuata huduma hiyo mjini.