Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Joyce Sokombi na Sussane Masele wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi mara baada ya kuhitimishwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Masele na Sokombi ni miongoni mwa wabunge wa Chadema waliotakiwa na Kamati Kuu ya Chadema kujieleze juu ya uamuzi wao wa kukiuka makubaliano ya chama ya kukaa karantini kwa siku 14 huku wenzao wanne wakitimuliwa uanachama.