Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha huko kwenye kitongoji cha Oloshoo kata ya Enguserosambu Tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro wamefanikiwa kukamata silaha ya kivita aina ya AK 47 yenye namba H 49 ikiwa na risasi 12 iliyokuwa njiani kufanya uhalifu kwenye Mbuga za wanyama.
Aidha kwa muktadha huo Mapambano dhidi ya matukio ya uhalifu na wahalifu ambapo kwa kipindi hichi wahalifu wengi hudhani jeshi la polisi limelala hivyo niwahakikishie hatujalala na tunaendelea kufanya misako na opereseheni mbalimbali iwe wakati wa mvua Jua Tope au Masika Baridi au kiangazi kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi ya kutenda uhalifu.
Akiongea na vyombo vya habari mkoani hapa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana alisema kuwa kikosi hicho kabambe baada ya kupewa taarifa fiche kuwa kuna watu 4 wawili watanzania na wakenya wawili wameonekana maeneo ya Mpakani wakiwa wanajipanga kuwinda wanyama adimu kwenye mbuga zetu muhimu.
Kwa mujibu wa Kamanda Shana baada ya kupata taarifa hizo kikosi kazi chenye askari machachari wazalendo na wenye weledi wa hali ya juu waliendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini juu ya taarifa hiyo na tarehe 10.6.2020 tulifanya msako mkali katika kijiji hicho kuwatafu wahalifu hao.
Alisema kuwa katika msako huo wahalifu wawili walikamatwa wakiwa na silaha moja ya kivita aina ya AK 47na risasi zake 12 ndani ya magazine ambao majina yao tunayahifadhi kwa ajili ya uchunguzi huku jeshi hilo likiendelea kuwatafuta watuhumiwa wawili waliokimbia nchi jirani ya Kenya.
Aidha jeshi la polisi linawasaka wahalifu hao kujisalimisha mara moja kituo chochote cha polisi kwani wasipofanya hivyo tutalazimika kutumia nguvu kubwa kuwatafuta ili hatua kali za kisheria zichukuliwe.
Kamanda Shana akatumia fursa hiyo kuendelea kuwashukuru wananchi ambao wameendelea kutoa taarifa mbalimbali za uhalifu na wahalifu huku akiwataka kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuwafichua wale wote wenye nia ovu ili kumaliza uhalifu kwenye mkoa wetu.
Amebainisha kuwa Jeshi hilo mkoani hapa linaahidi litatoa donge nono kwa yeyote atakaye toa taarifa zitakazo fanikisha kuwakamata wahalifu wanaojihusisha na Uwindaji haramu ,Ujambazi ,na uhalifu wa aina yeyote.