Waziri wa Nishari, Dkt. Medard Kalemani( kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela( kulia) wakiteta jambo baada ya waziri wa nishati, kufanya ziara katika ghala la kuhifadhi na kupokea mafuta Kampuni ya GBP mkoani Tanga, Mei 10, 2020.
Kamishna wa Maendeleo Petroli wa Wizara ya Nishati, Adam Zuber( kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa pamoja nchini( PBPA) erasto samwel( katikati) walimsikiliza Waziri wa Nishari, Dkt. Medard Kalemani,( hayupo pichani) akizungumza baada ya kufanya ziara katika ghala ya kuhifadhi na Kupokea mafuta Kampuni ya GBP mkoani Tanga, Mei 10,2020.
Waziri wa Nishari, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia)akipita kukagua mazingira ya ghala la kuhifadhi na kupokea mafuta la kampuni ya GBP, alipofanya ziara katika eneo hilo mkoani Tanga, Mei 10, 2020.
Shehena ya Mafuta ikiwa imepakiwa katika matangi tayari kwa kusafirishwa,hapa ni katika ghala la kuhifadhi na kupokea mafuta la kampuni ya GBP mkoani Tanga, Waziri wa Nishari, Dkt. Medard Kalemani, alifanya ziara katika eneo hilo, Mei 10,2020.
Baadhi ya mapipa makubwa ya kuhifadhia mafuta katika ghala la kuhifadhi na kupokea mafuta la kampuni ya GBP mkoani Tanga, Waziri wa Nishari, Dkt. Medard Kalemani, alifanya ziara katika eneo hilo, Mei 10, 2020.
Muonekano wa eneo kitakapojengwa kifaa cha kupimia mafuta (Flow Meter) kutoka katika meli hadi katika maghala ya kuhifadhi na kupokea mafuta katika bandari ya Tanga, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, alifanya ziara katika eneo hilo, Mei 10, 2020.
Waziri wa Nishari, Dkt. Medard Kalemani, (katikati) akiwasha umeme katika moja ya Ofisi za Serikali ya Kijiji katika Kijiji cha Mbuyuni Kata ya Mapatano wilayani Mkinga, mkoani Tanga, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini katika wilaya hiyo, Mei 10, 2020.
………………………………………………………………………..
Na Zuena Msuya Tanga,
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, ametoa siku kumi kwa Mamlaka
ya Udhibiti huduma za Nishati na Maji (EWURA) kumpatia majibu ya
uwiano wa viwango vya bei ya mafuta katika maghala ya Kupokea na
kuhifadhia mafuta nchini.
Dkt. Kalemani alisema hayo alipofanya ziara ya kutembelea ghala la
kuhifadhia mafuta la kampuni ya GBP iliyoko mkoani Tanga, Mei 10, 2020,
ili kuona kama agizo lake alilolitoa mwezi Machi, 2020, la kuwataka
waagizaji mafuta nchini wanaagiza shehena kubwa kutokana na tishio la
kuwepo kwa virusi vya Corona.
Pia alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini
katika wilaya ya Mkinga na Muheza mkoani huo pamoja na kuwasha
umeme.
Baada ya kupata taarifa ya mwenendo wa uingizaji,upokeaji na uhifadhi wa
mafuta nchini katika maghala pamoja na mambo mengine, Dkt.Kalemani
aliiagiza EWURA kufanya tathmini ya bei ya mafuta katika maghala hayo
kwa lengo la kuboresha biashara ya mafuta kwa maslahi ya watumiaji na
wafanyabiashara.
Dkt.Kalimani alisema kuwa, serikali imeweka utaratibu wa kuweka maghala
ya kupokea na kuhifadhi mafuta katika kila ukanda wa nchi kwa lengo la
kuwapunguzia gharama za usafiri wafanyabiashara wa mafuta
wanaotembea umbali mrefu kuyafuata mafuta hayo, pia kuwezesha
watumiaji kupata huduma hiyo kwa haraka, karibu na kwa bei nafuu wakati
wote.
Sambamba na hilo kulinda ubora wa miundombinu ya barabara nchini kwa
kuwa magari yanayobeba mizigo mizito ikiwemo mafuta yamekuwa
yakichangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa barabara.
“EWURA na PBPA nawapa siku 10,muangalieni uwiano na uratibu sahihi
wa bei ya mafuta katika maghala ili bei hizo zisitofautiane sana na taratibu
za bei zilizowekwa, kwa kuwa mafuta yapo mengi nayakutosha, na
mniletee majibu, Lengo la serikali ni kuhakikisha mafuta yanapatikana kwa
urahisi na kwa bei nafuu wakati wote kwa kuwanufaisha wafanyabiashara
na watumiaji”, alisema Dkt. Kalemani.
Alitoa wito kwa wafanyabiashara wa mafuta kwa kanda ya kaskazini
ikiwemo Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Tanga kutumia ghala la
kuhifadhi na kupokea mafuta lililopo mkoani Tanga kuliko kuyafuata mkoani
Dar Es Salaam.
“Wafanyabiashara wanaofuata mafuta Dar es salam watalazimika kuuza
kuwauzia watumiaji kwa bei ya juu hivyo kuwakandamiza watumiaji hii si
sahihi na ndiyo maana karibu kila ukanda wa nchi tumeweka ghala la
kuhifadhi na kupokea mafuta,tofauti na ilivyokuwa awali mafuta yote
yalikuwa yakipatikana mkoani Dar Es Salaam pekee”,alisisitiza Dkt.
Kalemani
Alitoa wito kwa makampuni yote ya uwagizaji wa mafuta nchini kwa
kushirikiana na EWURA na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja
(PBPA)kushirikiana kwa pamoja kuendelea kuleta mafuta mara dufu ili
kujihakikishia uwepo wa mafuta nchini hata kama ugonjwa wa corona
utaendelea kuwepo.
Dkt. Kalemani alifafanua kuwa mafuta yaliyopo nchini kwa sasa yanauwezo
wa kutumika zaidi ya miezi miwili hadi mitatu mbele na bado kila siku
wanapokea mafuta, ambapo kwa sasa nchi inapokea inapokea mafuta lita
milioni 428.7 tofauti na awali kabla ya agizo kutoka ilikuwa ikipokea mafuta
lita milioni 185.
Aidha aliwataka wafanyabiashara ya mafuta kujenga vituo vya mafuta
katika maeneo yaliyo vijijini ili kulinda ubora wa mafuta na kusogeza
huduma karibu na watumiaji hasa wadogo akitolea mfano waendesha
pikipiki ambao ndiyo wanaotegemeo kubwa la usafiri katika maeneo ya
vijijini.
Alisema kuwa watumiaji wadogo wa vyombo vya moto, wamekuwa
wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya mafuta, na wengine
wamekuwa wakihifadhi mafuta katika nyumba zao jambo ambalo
linahatarisha usalama wao.
Aidha alisema kuwa pia kumekuwa na tabia ya kuuza kiholela mafuta na
uhifadhi mbovu wa mafuta hayo na hivyo kupunuza ubora waviwango vya
mafuata kwa watumiaji na hivyo hata kulazimu mafuta hayo kuchanganywa
na hivyo kuchangi uharibifu wa yyombo vinavyotumia mafuta hayo.
“Wafanyabiashara nendeni mkajenge vituo vidogo vya mafuta vijijini,
mrahisishe huduma ya upatikanaji wa mafuta na bei nafuu kwa watumiaji
wadogo ambao wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma
hiyo,tuungane kutekeleza lengo la serikali la kuhakikisha kila mtumiaji wa
mafuta anapata bishaa hiyo kwa wakati na kwa bei nafuu”, alisisitiza Dkt.
Kalemani.
Pamoja na mambo mengine alitembelea eneo inapojengwa kifaa
kitakachotumika kupima mafuta (Flow Meter), yanayoingia nchini kutoka
katika Meli kwenda katika maghala ya kuhifadhi na kupokea mafuta katika
Bandari ya Tanga.
Aliiagiza mamlaka ya bandari nchini kukamilisha ujenzi wa mtambo huo
haraka ili serikali ipate kiwango sahihi cha mafuta yanayoingia nchini
kupitia Bandari ya Tanga ili kupata kodi na tozo stahiki.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uagizaji mafuta ya
GBP, Badar Seif Sood alimueleza Waziri wa Nishati kuwa wamefanya
upanuzi wa bandari hiyo, hivyo kwa sasa inauwezo wa kuhifadhi na
kupokea mafuta lita milioni 182, tofauti na walivyokuwa wananza mwaka
2017 walipokuwa wakihifadhi na kupokea mafuta lita milioni 182, na
upanuzi utaendelea kulingana na mahitaji.
Aliishukuru serikali kupitia wizara ya nishati, kuendelea kuwalinda
wafanyabiashata wa mafuta wakiwamo wamiliki wa maghala ya kuhifadhi
na kupokea mafuta pamoja na waagizaji wakubwa wa mafuta kwa
kuhakikisha wanafanya biashara zao katika mazingira rafiki: Huku akiahidi
kuendelea kutoa huduma bora kwa watumiaji wa mafuta hayo nchini.
Katika ziara hiyo, Dkt. Kalemani, pia alikagua maendeleo ya usambazaji
wa umeme vijijini katika Wilaya ya Mkinga na kuwasha umeme katika kijiji
cha Mbuyuni kata ya Mapatano na kutembelea kisima cha maji katika kijiji
cha Jihirini na kuliagiza Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kupeleka na
kuwasha umeme katika kisima hicho mwishoni mwa mwezi huu.
Vilevile alitembelea Wilaya ya Muheza na kukagua kazi ya usambazaji wa
umeme katika kijiji cha Kwakokwe na kuwataka wananchi kuendelea
kulipia gharama za kuunganishiwa umeme kwa kuwa vijijini vyote nchini
vitapata umeme na kwamba wasikubali kuuziwa miundombinu ya umeme
na pia watumie wakadarasi wanaotambulika na TANESCO katika
kutandaza nyaya katika nyumba zao.