Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde akizungumza na familia ya mchungaji Yoram Isihaka wa Kanisa la United Methodist Mbabala B ambaye analea watoto Yatima baada ya kuwasili katika Kata ya Mbabala iliyopo Jijini Dodoma leo.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde akipata maelezo kutoka kwa mchungaji Yoram Isihaka wa Kanisa la United Methodist Mbabala B ambaye analea watoto Yatima baada ya kuwasili katika Kata ya Mbabala iliyopo Jijini Dodoma leo.
Msaada wa mahitaji muhimu aliyo leta Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde kwa mchungaji Yoram Isihaka wa Kanisa la United Methodist Mbabala B ambaye analea watoto Yatima baada ya kuwasili katika Kata ya Mbabala iliyopo Jijini Dodoma leo
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde akikabidhi msaada wa mahitaji muhimu kwa mchungaji Yoram Isihaka wa Kanisa la United Methodist Mbabala B ambaye analea watoto Yatima katika Kata ya Mbabala iliyopo Jijini Dodoma leo
………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde amekabidhi msaada kwa Mchungaji Yoram Isihaka wa Kanisa la United Methodist Mbabala B Kata ya Mbabala Jijini Dodoma ambaye anawalea watoto yatima kutoka maeneo mbalimbali ya Dodoma bila kujali dini zao.
Msaada huo ni magodoro 20,Sukari kilo 40,Sabuni boksi 10,Unga wa Sembe kilo 100,Sabuni za Maji lita 40,tende boksi 5 ,madumu manne ya kunawia,Tofali 2000 na saruji mifuko 20 kwa ajili ya ujenzi wa bweni jipya la watoto.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Mavunde amesema kuwa Mchungaji Yoram amekuwa akiwatunza watoto hawa kwa nyumba iliyokuwa imejengwa kwa udongo.
Aidha Mavunde amesema kuwa baada ya mvua kubwa za mwaka huu nyumba hiyo ilidondoka na hivyo watoto hao pamoja na Mchungani kukosa malazi hatua ambayo ilimlazimu kuligeuza kanisa kama nyumba ya kuwahifadhi watoto hao na kuwaomba waumini wasali chini ya mti mpaka hali itakapotengamaa.
“Duniani kila mtu amekuja hapa kwa kusudi la Mungu,kuna watu uwepo wao hapa duniani ni faraja sana kwa watu wengine na leo nimestaajabu sana juu ya hali ya upendo,kujali na huruma !”, amestaajabu Mavunde
Mavunde ameeleza kuwa alifikishiwa habari hii na Vijana wa Kata ya Kilimani ambao na wenyewe waliguswa na haya maisha ya Mchungaji na kuomba niwaunge mkono katika mchango waliokuwa wakichangishana nilikubali kwa moyo mmoja kutimiza haya ya watoto hawa wa Mungu.