Home Mchanganyiko RC MAKONDA ATOA SHEHENA YA FUTARI KWA MAKUNDI YA WATU WASIOJIWEZA.

RC MAKONDA ATOA SHEHENA YA FUTARI KWA MAKUNDI YA WATU WASIOJIWEZA.

0

**************************************

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa shehena ya Futari ikiwemo Sukari, Mchele, Unga, Maharage na Mafuta kwa zaidi ya Watu 350 kutoka Makundi mbalimbali ikiwemo Yatima, Walemavu wa Viungo, Wasioona, Watu wenye ulemavu wa Ngozi Albino na Watu wasiojiweza kama sehemu ya sadaka ya Mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Katika Shehena hiyo aliyotoa RC Makonda kila Mwananchi amepata vifurushi vyenye Mchele Kilo 5, Unga kilo 5, Sukari, kiroba cha Maharage na Mafuta ya kupikia.

Msaada huo wa Futari aliotoa RC Makonda umetoka kwenye Taasisi ya MIRAAJ TANZANIA iliyompatia Vitu hivyo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zake na RC Makonda akaelekeza vitu hivyo vitolewe kwa watu wa wasiojiweza katika jamii ili Waweze kupata ahueni Kipindi hiki cha Mfungo.

Akitoa Futari hiyo kwa walengwa kwa niaba ya RC Makonda, Mkurugenzi wa Taasisi ya Miraaj Tanzania Bw. Arif Tanzania amesema Taasisi hiyo imekuwa na imani kubwa na Mkuu wa Mkoa kwakuwa kila msaada anaopatiwa anaufikisha kwa walengwa tena kwa uwazi Mkubwa.

Aidha Bwana Arif amesema Taasisi hiyo itaendelea kumuunga mkono RC Makonda katika kila jambo kwakuwa amekuwa kiongozi anaegusa maisha ya Watu wa Makundi mbalimbali ndani ya Jamii.