Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed kushoto akimkabidhi vyakula vya futari na vifaa vya kujikinga na Ugonjwa wa Corona Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee vyenye thamani ya milioni 16 vilivyotolewa na Kampuni ya Mafuta ya GP mapema leo kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Makorora Ramadhani Badi
Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee kushoto akibidhi mmoja wa wananchi wa Kata ya Makorora Futari yenye thamani ya milioni 16 vilivyotolewa na
Kampuni ya Mafuta ya GP mapema leo ikiwemo vifaa vya kujikinga na Virusi vya Corona
Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee kulia akikabidhiwa vitakasa mikono (Sanitize ) na vyakula kutoka kwa Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed vyenye thamani ya milioni 16 vilivyotolewa na Kampuni ya Mafuta ya GP mapema leo
Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee kulia akigawa msaada huo kwa wananchi wa mitaa mbalimbali kwenye Kata hiyo kulia ni Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed
Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed akiwaaonyesha waandishi wa habari vitakasa mikono ambavyo vimetolewa
***************************
DIWANI wa Kata ya Makorora Jijini Tanga (CCM) Omari Mzee ameishukuru Kampuni ya Mafuta ya GP kwa kutoa msaada futari kwa kaya 150 kwenye kata yake ikiwemo vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Huku akiwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuwaelimisha watoto wao ili kuona ile mikusanyiko isiyokuwa ya lazima waweze kuepukana nayo ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na Ugonjwa wa Virusi vya Corona ambayo kwa sasa vinaitikisha dunia.
Omari aliyasema hayo leo wakati akipokea msaada huo wenye thamani ya Milioni 16 vilivyotolewa na kampuni ya Mafuta ya GP vilikabidhiwa na Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed kufuatia ombi la kumtaka ashirikiana nao kwenye kukabidhi vyakula na vifaa hivyo..
Alisema vifaa hivyo vitawasaidia wakati huu wa mwezi wa ramadhani ikiwemo katika kukabiliana dhidi ya Ugonjwa huo wa Corona huku akiwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ambazo zimekuwa zikitolewa na wataalamu wa Afya hapa nchini.
Aidha alisema kwa sasa shule zimefungwa na watoto wamekuwa wakizagaa mitaani hivyo wanapaswa kuchukua tahahdari kwa kuwaelimisha ili kuona ile mikusunyiko ilisyokuwa ya lazima waweze kuepukana nayo kwa lengo la kuwaepusha na maambukizi ambayo wanaweza kukumbana nayo.
“Nishukuru sana kwa furari hii kwa zile kaya ambazo hawajiwezi zitawasaidia kupunguzia makali ya maisha lakini wazazi tutambue ugonjwa huu wa Virusi vya Corona upo hivyo niwasihi wazazi na jamii nzima kwa ujumla tuweza kuchukua tahadhari kukabiliana nao “Alisema Diwani huyo.
Awali akizungumza kabla ya makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed alisema kwamba wamekabidhi vyakula hivyo kwenye
kaya masikini 150 ambavyo vimetolewa na kampuni.
Ambapo alisema kutokana na ukongwe wangu wa kampuni za Oili Mkoa wa Tanga wamemuomba washirkiane nami kukabidhi vyakula hivyo kwa waliofunga mwezi mtufuku na vifaa vya kujikinga dhidi ya Corona vyenye thamani ya milioni 16.
Vifaa hivyo alivikabidhi kwa diwani wa Kata hiyo
Omari Mzee ili aweze kuvikabidhi kwa wananchi kwenye mitaa ili kuweza kuwapunguzia makali ya maisha waliokuwa nao baadhi ya jamii maeneo hayo kutokana na kushindwa ukata ambao wamekuwa wakikumbana nao.