Home Biashara TBL Plc yaunga mkono Serikali kupambana na COVID 19 kwa kuzalisha vitakasa...

TBL Plc yaunga mkono Serikali kupambana na COVID 19 kwa kuzalisha vitakasa mikono

0

Waziri wa Afya,Jinsia ,Wazee na Watoto,Mh.Ummy Mwalimu (katikati) akipokea msaada wa lita 618 za vitakasa mikono kutoka kwa Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa kampuni ya TBL Plc ,Georgia Mutagahywa, (Kulia) vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya vituo vya afya kwa ajili ya kupambana na Corona (kushoto) ni mwenyekiti wa TPSF,Angelina Ngalura

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu (katikati) akipokea msaada wa vitakasa mikono kutoka kwa Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa kampuni ya TBL Plc, Georgia Mutagahywa, (wa pili kulia )vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya vituo vya afya nchini kwa ajili ya kupambana na  virusi vya ugonjwa wa  Corona (COVID 19 ) wengine kutoka kushoto ni mwenyekiti wa TPSF,Angelina Ngalura,Meneja Mawasiliano wa TBL Plc, Amanda Walter na Meneja wa Masuala Endelevu TBL Plc, Abigail Mutaboyerwa.

*******************************

 
-Yatoa msaada wa lita 618 kwa Wizara ya Afya

Kampuni ya TBL Plc,  imetoa msaada wa lita 618 za vitakasa mikono kwenye  vifungashio vya  lita 5, kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya matumizi ya vituo vya afya kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.

Akiongea jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi msaada huo kwa Waziri wa Afya, Mh.Ummy Mwalimu, Mkurugenzi mkuu wa TBL Plc, Philip Redman, alisema,vitakasa mikono hivyo zilizotengenezwa kwa malighafi yenye kilevi vimetengenezwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya Diversey East and Central Africa Limited.

Redman, aliongeza kusema kuwa shehena nyingine ya vitakasa mikono vilivyotengenezwa na kampuni yake vitakabidhiwa kwa Serikali siku chache zijazo “Tumepata ombi la kutoa msaada kwenye vifaa vya kinga na  bado tunafanya jitihada kutoa msaada wa vifaa hivyo pia”,alisema Redman.

Mbali na kutengeneza vitakasa mikono kwa ajili ya kutumiwa katika vifaa vya afya.TBL pia imetengenezwa kifurushi cha vifaa  vya kinga ya COVID 19 (COVID 19 kits) ambavyo vitagawiwa kwa wateja wake, ambapo kila kifurushi kitakuwa na mililita 500 za vitakasa mikono ,barakoa nne za vitambaa na kitabu cha maelezo ya jinsi ya kutumia barakoa kujikinga na ugonjwa.

Kwa upande wake Waziri wa Afya,Mh.Ummy Mwalimu,alitoa shukrani kwa wadau wote ambao wanaendelea kuonyesha moyo wakuunga mkono jitihada za Serikali za kukabiliana na ugonjwa wa COVID 19 kwa kutoa misaada kupitia kamati ya Taifa ya kupambana na ugonjwa huo.

TBL ina historia ya muda mrefu ya kutoa mchango wa kusaidia kukuza uchumi wa kijamii nchini Tanzania kupitia sekta za kilimo,usafirishaji na viwanda.