Afisa Mtendaji Kata ya Mazimbu, Prisca Mawala (kulia) akimpa maelekezo , Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga jinsi ya kutafuta majina na kufanya uhakiki kwenye ubao
wa matangazo wa Kata ya Mazimbu ambapo ndipo alipojiandikishia.
Mstahiki Meya wa Manispaa Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga (kushoto) akifanya uhakiki wa
Kitambulisho cha kupigia kura.
.Mhe. Kihanga akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuhakiki taarifa zake katika
Daftari la Uboreshaji la wapiga kura
Baadhi ya Majina ya waliojiandikisha awamu ya kwanza katika Daftari la wapiga kura , ambapo
miongoni mwao ni taarifa za Mstahiki Meya , Mhe. Pascal Kihanga zikionekana kwenye ubao wa
matangazo.
*********************************
Na Farida Saidy,Morogoro
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga,
amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Awamu ya pili ya Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura na kuwahimiza Wananchi waliotimiza miaka 18 na wale ambao
walishajiandikisha awamu ya kwanza wajitokeze kwa wingi kuhakiki taarifa zao ili kutimiza haki zao za
kuwachagua viongozi wanaowataka katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka 2020.
Kihanga , ameyasema hayo leo Mei 2, 2020 Kwenye Ofisi ya Kata ya Mazimbu wakati alipokwenda
kuhakiki taarifa zake kwenye Kituo alichojiandikishia kilichopo Mtaa wa Modeco 'B' .
Aidha, amewata Madiwani wote kutumia fursa hii kuwaagiza Wenye Viti wao wapitie nyumba hadi
nyumba kuwahimiza Wananchi wao kwenda kuhakiki taarifa zao kwani muda uliopo sio rafiki.
“Tuna muda mchache sana, leo Jumamosi na Jumapili ni siku za mapumziko , kwa Wafanya kazi na wale
watumishi wazitumie siku hizi kikamilifu kuhakiki taarifa zao ili itakapoanza Jumatatu siku za kazi basi
waendelee na majukumu yao mingine , muda sio rafiki kwentu siku hizi 3 sio nyingi sana, niwaombe
tusidharau lazima mtambue kwamba zoezi hili ni muhimu sana , mimi nimehakiki taarifa zangu lakini
Picha haipo kwahiyo ikanibidi nikapige picha upya na kupewa kitambulisho changu kipya, ukidharau
unaweza ukajikuta unapoteza sifa za mpiga kura katika uchaguzi” Amesema Kihanga.
“Zoezi hili limeanza lazima Wananchi walipe kipaumbele na kuacha dharau, napenda kuwaomba
Wananchi wa Manispaa ya Morogoro kwenye Kata zote 29, wajitokeze kwa wingi kwani zoezi hili
linahusika na uandikishaji wa wapiga kura wapya wenye sifa ili waweze kupata fursa za kushiriki kupiga
kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka 2020” Amesisitiza Kihanga.
Pia amewaomba wale wananchi waliohama kutoka eneo moja kwenda jengine waende katika Vituo
walivyopo kwa sasa ili waweze kuhamisha taarifa zao katika Daftari la wapiga kura ili waweze kushiriki
kikamilifu katika kuwachagua Viongozi katika uchaguzi Mkuu.
Hata hivyo, amesema wapo wale ambao wamefikisha umri wa miaka 18 au wanafikisha mwaka huu
kabla ya Mwezi Oktoba, waende katika Vituo ili waweze kurekebisha taarifa zao na wale ambao
wamehama Mkoa, eneo nje ya Kata pamoja na kutoka Jimbo moja kwenda jengine wote wanatakiwa
wakahakikihi taarifa na kuweza kuhamisha taarifa zao.
Hata hivyo ameendelea kutoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Morogoro kuendelea kufuata ushauri
wa Wataalamu wa Afya katika kujikinga na Ugonjwa wa Corona ikiwemo kunawa Maji tiririka na sabuni,
kutumia Vitakasa mikono ( Sanitizer), pamoja na kuepuka msongamano isiyo ya lazima na kukaa
nyumbani kama mtu hana sababu ya Msingi ya kutoka
Naye , Afisa Mwandikishaji Msaidizi wa Jimbo Morogoro Mjini, Waziri Kombo , amesema bado
hajaridhishwa na Mwitiko wa watu , hivyo amewataka Wananchi kuacha kupuuzia swala hilo kwani
wasipofanya hivyo kuna hatihati ya wale ambao taarifa zao hazitakuwa sahihi au kutoonekana kwa picha
zao wakapoteza sifa ya kupiga kura.
Katika hatua nyenge, Kombo,amesema kumekuwa na changamoto ya kutoonekana kwa picha za watu
katika Vituo, hivyo wananchi wanatakiwa watambue uhakiki ni jambo muhimu sana ili waweze kuwa na
sifa za kupiga kura.
“Serikali inajicho pana , ndio maana kuna zoezi la uhakiki, ukiangalia changamoto kubwa ambayo
nimeiona ni kutokuonekana kwa picha za watu katika majina yao waliyojiandikisha mwanzo, niwaombe
wale ambao wanashida hiyo wakapige picha upya kwenye vituo vilivyowekwa, na uhakiki pia ni muhimu
ili changamoto hii iweze kupatiwa ufumbuzi , kama tutadharau ujue kabisa utajipotezea sifa ya kuwa
mpiga kura na kukosa haki yako ya msingi na ya kikatiba” Amesema Kombo.
Kombo, amewataka waandikishaji kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo la Uboreshaji wa Daftari la
kudumu la wapiga kura awamu ya pili na kutekeleza zoezi hilo kwa kwa umakini na ufanisi pamoja na
utunzaji wa vifaa vyote vitakavyohusika katika zoezi hilo.
Amesema matarajio yake ni kuona zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga Kura linafanikiwa
kwa kiwango kikubwa ili kuwa na taarifa sahihi za wapiga Kura.
Pia amesema njia mbadala zitakazotumika katika uhakiki wa daftari ni kama zifuatazo;
I. Bonyeza *152*00#ok
II. Chagua Namba 9 ambayo ni Uchaguzi Mkuu
III. Chagua tena Namba 1 ambayo ni Uhakiki Taarifa za Mpiga Kura
IV. Baada ya hapo unatakiwa kuingiza Namba ya Mpiga Kura (Utaweka Namba peke yake bila ya
herufi (T) wala , Dash (-)
Kwa upande wa Afisa Mtendaji wa Kata ya Mazimbu, Bi. Prisca Mawala, amesema kwa upande wa Kata
ya Mazimbu wamewahamasiha sana Wananchi kwa kutumia gari la mapatangazo hivyo matarajio yake
hizi siku mbili mahudhurio yataongezeka huku akiomba uhamasishaji zaidi kupitia kwa Wenyeviti wa
Mitaa na wajumbe wao