…………………………………………………………..
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
DUKA la dawa linalomilikiwa na hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, linasaidia upatikanaji dawa kirahisi kwa wagonjwa wanaofika kwa ajili ya huduma ya tiba,ambapo lilipata mkopo wa dawa za sh.milioni 50 kutoka MSD, na kufanikiwa kupata sh. milioni 36.
Duka hilo lililoanzishwa kwa mtaji wa sh.milioni 4, walianza kununua dawa muhimu na za lazima kwa wateja wa Bima.
Hayo yalielezwa na Mganga Mkuu wa wilaya (DMO) Dr Aziz Msuya mbele ya viongozi wa halmashauri ya wilaya, waliofika kuangalia shughuli zinazofanywa hospitalini hapo.
Alisema, utekelezaji wa agizo la serikali Kuu za kuzitaka hospitali na Vituo vya afya kuwa na duka la dawa, na kwamba tayari wameshailipa MSD kiasi hicho cha fedha kupitia duka hilo la jamii, lililobadilishwa kutoka duka la dawa la Bima na kuwa la jamii.
“Duka hili linalotoa huduma kwa wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya, limekuwa kivutio kwa wateja wengine wa kawaida waliokosa dawa kwenye duka la utaratibu wa kawaida, ambalo linasaidia wananchi waliokuwa wananunua dawa nje,” alisema.
“Mpaka sasa kupitia duka la Bima, huduma za afya zimeimarika kwani dawa zinapatikana kwa asilimia 97, ambapo fomu zilizokuwa zinatoka nje zimepungua, na kwa baadhi ya siku kutokuwepo kabisa sanjali na upatikanaji wa uhakika wa dawa,” alisema Msuya.
Aidha dr
Msuya alieleza mapato yameimarika kutoka sh.milioni nne wakati wanaanzisha mpaka milioni 85 ikiwa ni mafanikio makubwa, ukilinganisha na mapato ya fomu ya Bima ya afya za madai yakiwa milioni 20 kwa mwezi wakati mwingine kushuka mpaka milioni 17 kutokana na kukosekana kwa dawa.
Kwa upande wake Mratibu wa Bima ya afya wilaya Dr Jane Mcharo, alisema kuwa uwepo wa duka hilo umeongeza mapato ya Bima ya afya kupitia fomu za madai kutoka milioni 35 au zaidi kwa mwezi na mapato taslimu katika duka pekee kufikia milioni 15 kwa mwezi.
Kwa upande wake Ally aliupongeza uongozi huo wa hospitali kwa juhudi inazozionesha katika uboreshaji wa huduma za tiba kwa wana-Bagamoyo, huku akisema kwamba halmashauri inatambua na kuthamini kazi zinazofanywa na wataalamu hao wa afya.