**********************
NA FARIDA SAIDY,MOROGORO
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo , amezindua
rasmi Wodi ya Wazazi ijulikanyo kwa jina la “Wodi ya Wazazi Regina
Chonjo” katika Kituo cha Afya cha Sabasaba Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo,
Mhe Chonjo, amewataka Wauguzi kutumia taaluma zao kwa uwaledi ili
Wazazi wajifungue salama.
Aidha, amekipongeza kituo hicho cha afya kwani tangia ianze huduma
ya uzalishaji haijawai kutokea kifo cha Mzazi wala Mtoto huku akisema
jambo hilo linastahili pongezi kwani Wauguzi wamekuwa makini na
wanazingatia waledi kazini.
“Kituo kizuri sana, kwanza hongereni nimesikia taarifa ikisomwa
kwamba tangia mtoe huduma hii ya kujifungua kwa Wazazi wetu,
hakuna matukio ya vifo, endeleeni hivyo hivyo kuwahudumia wazazi
vizuri, mimi sitegemei kupata malalamiko hadi Wazazi wakaanza
kukimbilia Vituo vyengine, mmeonyesha mnaweza na sisi
tunawategememea katika kutoa huduma bora na kuwafanya Wakina
mama kuja kwa wingi katika Kituo chetu kutokana na ubora wa huduma
zinazopatikana hapa” Amesema Chonjo.
Amesema lengo la Serikali kujenga Jengo hilo la Wodi ya Wazazi ni
kuwawezesha Wananchi (wakina mama wajawazito ) kupata huduma za
kujifungulia karibu na makazi yao ili kupunguza vifo vya Mama
Wajawazito na Watoto pamoja na kuwapunguzia umbali wa kufuata
huduma za afya Hospitali ya Mkoa.
Amesema Ujenzi wa Wodi hiyo umegharimu jumla ya Shilingi Milioni
129,923,180/= ambapo fedha hizo zinajumuisha gharama za Ujenzi,
dawa pamoja na vifaa tiba.
DC Chonjo, amelishukuru sana Baraza la Madiwani linaloongozwa na
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga,
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba pamoja na
Watumishi wote wa Manispaa kwa kazi nzuri walioifanya kwa
kuzingatia maelekezo na maagizo hadi wakaipa jina lake Wodi hiyo
jambo ambalo limemfanya ajisikie furaha na limeendelea kumpa
heshima kubwa na kuacha alama katika utawala wake katika upande wa
afya.
Katika hatua nyengine, DC Chonjo, amepongeza hatua zilizochukuliwa na Manispaa ya Morogoro kufuatia agizo lake la kutaka Manispaa hiyo kutengeneza Vitakasa mikono kwa kutumia malighafi ya ndani kama alivyosisitiza Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Amesema Vitakasa mikono vitauzwa kwa bei elekezi ya Shilingi 2500/= kama alivyoelekeza ili kila mwananchi awe na uwezo wa kununua ukilinganisha bei ya dukani kuwa juu sana.
Hata hivyo, DC Chonjo , amechukizwa na baadhi ya Wazazi kushindwa kuwafungia Watoto wao ndani wakati Serikali ilishatoa mapumziko kwa
Wanafunzi katika janga hili la CORONA.
Amesema jukumu la ulinzi wa Mtoto nyumbani ni la Wazazi/Walezi
lakini bado watoto wanazurura hovyo , unaweza kuta baada ya kurudi
shule wanafunzi hawa nusu yake wakawa Wazazi katika Wodi ya
Regina Chonjo.
Pia DC Chonjo, amepiga marufuku na kuwaomba wakulima wa vyakula
kuacha tamaa ya kuuza vyakula vyao vikiwa vichanga mashamabani
badlaa yake waviache ili kuweka akiba ya chakula kukwepa kukaribisha
njaa siku za usoni.
Mwisho , DC Chonjo, ameuomba Uongozi wa Manispaa ikiwemo Baraza la Madiwani, pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi kuona haja ya kuongeza Jengo la Chumba cha upasuaji ili kuendelea kuokoa maisha ya Wakina mama mara wanapopata shida kubwa kwani Hospitali ya Mkoa
ipo mblai inaweza kupelekea kupoteza maisha ya wakina mama wakati wa kuwakimbiza hositali kubwa.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, amesema kuwa
Manispaa imejitahidi kuimarisha Vituo vya afya hususani katika Wodi
za Wazazi ili kuhakikisha mama wajawazito wanazaa kwa usalama bila
kupoteza maisha.
Amesema kutokana na ombi la Mkuu wa Wilaya ya kutaka kuongeza
Jengo la Chumba cha upasuaji amelipokea na atalifikisha katika vikao
vya Baraza ili katika mwaka mwengine wa fedha 2021/2022 waweze
kuliingiza katika bajeti.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Fikiri Juma,
ameipongeza Manispaa ya Morogoro kwa utekelezaji wa Miradi mingi
iliyomalizika na inayoendelea kutekelezwa.
Amesema ameshuhudia Maboma ya Shule za Sekondari na Msingi
yakimalizika , Vituo vya afya, Ofisi za Watendaji hii imetokana na
Manispaa kutekeleza vyema na kwa viwango vya kisasa Ilani ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM ).
“Kikubwa zaidi ,, nimefurahishwa na jina la Wodi hii, kiukweli Manispaa mmemtendea haki Mama yetu Regina Chonjo, amekuwa mstari wa mbele sana katika kuchochea maendeleo katika Wilaya yetu, tangia tuwe naye mwaka 2016 yapo mengi mazuri yamefanyika na
tumeona uongozi wake uliotukuka, ningeshangaa sana jina lake lingekuwa katika Jengo baya, yeye ni DC wa Viwango na Jengo pia lina
viwango”Amesema Fikiri.
Kwa upande wa Afisa Muuguzi wa Kituo afya Sabasaba, Dr. Vulfrida
Kyara, amesema jengo hilo lilifunguliwa Agosti ,2019 likiwa na uwezo
wa kuhudumia wakina mama 18 kwa wakati mmoja huku lengo likiwa
ni kuwahudumia wakinana wapatao 2585 wa Kata ya sabasaba lakini
mpaka sasa ina hudumia zaidi ya hao huku wengine wakiwa wanatokea
Kata mbalimbali za Manispaa na nje ya Manispaa.
Amesema mpaka sasa wakina mama waliolazwa katika wodi hiyo
wamefikia 965, ambapo kati ya hao waliojifungulia Kituoni hapo ni
wakina mama 714 sawa na asilimia 74% na wakina mama 251 sawa na
asilimia 26% walipewa rufaa kwenda Hospitali ya Mkoa kwa ajili ya
huduma zaidi kubwa ikiwa ni huduma ya upasuaji ambayo haipatikani
kituoni hapo lakini katika kipindi chote cha huduma hakuna kifo cha
mama mjamzito kilichotokea .
Aidha, amesema pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika
utoaji huduma , zipo chanagamoto ikiwemo kukosekana kwa chumba
cha upasuaji hali inayosababisha rufaa nyingi zisizo za lazima, ukosefu
wa chumba maalum na vifaa kwa ajili ya watoto pamoja na ukosefu wa
Jenereta kubwa lenye uwezo wa kukidhi mahitaji hivyo kupelekea
ugumu wa huduma pale umeme unapokatika.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispa ya Morogoro, Waziri Kombo, amesema Jengo hilo limezinduliwa kwa jina la Regina Chonjo , imetokana na mchango na uwezo wake mkubwa wa kuchangia maendeleo ya Wilaya zikiwemo huduma za Afya.
Amesema Uongozi wa Manispaa ya Morogoro, Watumishi wa Kituo cha Afya Sabasaba, Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Sabasaba pamoja na Kamati ya usimamizi wa Kituo kwa niaba ya Wananchi wamefarijika sana kwa heshima kubwa aliyotoa DC Chonjo kwa kukubali Jengo hilo liitwe kwa jina lake ambapo tukio hilo litabakia kuwa kumbukumbu
kubwa isiyofutika.
Kuhusu Vitakasa Mikono, akielezea na kutoa taarifa, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr Ikaji Rashidi,amesema kutoka na bei za Vitakasa mikono kuwa ghali kiasi cha kushindwa wananchi wa kawaida
kumudu na kuduwaza wananchi wa hali ya chini kupambana na maambukizi ya Virusi vya CORONA, wakaona ni vyema kuja na mpango huo ambao DC Chonjo aliwaagiza kuufanya.
Amesema ujio wa vitakasa Mikono vinavyojulikana kwa jina la MOROGORO MC Hand rub Sanitizer umezingatia viwango vilivyoelekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na vitauzwa kwa gharama nafuu ili kila mwananchi aweze kumudu kununua bidhaa hiyo na kushiriki vyema katika Vita dhidi ya Ugonjwa wa CORONA.
“Wazo hili la kutengeneza Vitakasa Mikono uliliagiza wewe, nichukue fursa hii kwa niaba ya Uongozi wa Manispaa ya Morogoro, kutamka kuwa maelekezo yako yametekelezwa ambapo leo unazindua bidhaa hii,
tunakupongeza kwa maono yako ambayo leo yamethihirika kuwa kweli (the dream come true), chupa ya ujazo wa Mls 100n itauzwa kwa Tsh 2,500/= amabpo katika maduka binafsi chupa ya ujzo huo inauzwa kati ya Tsh 4,000/= hadi 5,000/=”.Amesema Dr Ikaji.
Aidha amesema muongozo wa utengenezaji wa vitakasa mikono bidhaa hizo umezingatia WHO Recommended Handrub Sanitizer Formulation kwa kuchanganya viamabata kama vile Alcohol 80%, Grycerine 1.45%
pamoja na Hydrogen Peroxide 0.1255 huku akisema kutokana na upatikanaji wa malighafi kuwa bei kubwa imepelekea bei hiyo kuwa ghali kidogo japo lengo ilikuwa ni kuuza kwa bei ya chini sana kutokana na upatikana upatikaji wa malighafi kama ungekuwa rahisi.
Amesema Manispaa ya Morogoro inaunga mkono kauli ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli ya kuhamasisha utengenezaji na matumizi ya bidhaa za ndani dhidi ya mapambano ya kujikinga na Ugonjwa wa COVID-19 ,
hivyo wanaomba ushirikiano zaidi kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili kuweza kutafuta masoko kwa ajili ya uuzajin wa bidhaa hizo.