Home Mchanganyiko SBL yotoa msaada wa vitakasa mikono kupambana na virusi vya Corona

SBL yotoa msaada wa vitakasa mikono kupambana na virusi vya Corona

0

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akipokea sehemu ya lita 1,250 za vitasa mikono kutoka kwa Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) John Wanyancha (kulia) ikiwa ni mchango wa Kampuni hiyo katika kupambana na ugonjwa wa homa ya mapafu maarufu kama Covid-19.

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akiongea muda mfupi baada ya kupokea msaasa wa lita 1,250 za vitakasa mkono uliotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ikiwa ni mchango wa Kampuni hiyo katika kupambana na ungonjwa wa homa ya mapafu maarufu kama Covid-19.

Mkurungenzi wa Mahusinao kwa Umma wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) John Wanyancha (kushoto) akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi 1,250 za vitakasa mikono ikiwa ni mchango wa Kampuni hiyo katika kupambana na ugonjwa wa homa ya mapafu au Covid-19.  Kulia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu

**************************************

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imeunga mkono mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa homa ya mapafu maarufu kama Covid-19 kwa kutoa msaada wa lita 1,250 za vitasa mikono.

 

Msaada huo umekabidhiwa kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

 

“Tunaamini msaada huu utawasaidia watakaoutumia kuwa salama dhidi ya virusi hatari vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya mapafu au Covid-19,” alisema Mkurugenzi wa
Mahusiano kwa Umma wa kampuni hiyo John Wanyancha.
Hii ni mara pili kampuni ya SBL inaiunga mkono Serikali katika Mapambano dhidi ya Covid-19.

 

Wiki mbili zilizopita, SBL ilishirikiana na Wizara ya Afya kusambaza vipeperushi vyenye kutoa elimu ya kujikinga na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya mapafu katika sehemu mbali mbali nchini na kuvikabidhi kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya mbali mbali.

 

Pamoja na mchango huo, Wanyancha alisema kampuni ya SBL inatoa vitakasa mikono na barakoa kwa wafanyakazi wake wa mauzo, kiwandani pamoja na wasambazaji wa bidhaa za kampuni hiyo waliopo sehemu mbali mbali nchini ili kuwawezesha kufanya kazi katika mazingira
salama. Kampuni ya SBL inawafanyakazi 800 na mamia ya wasambazaji waliotapakaa kila kona ya nchi.

 

Akipokea msaada huo, Waziri Mwalimu aliishukuru kampuni ya SBL kwa kuiunga mkono Serikali
katika vita dhidi ya virusi vya Corona na kusisitiza kuwa vita hiyo inahitaji kuunganisha nguvu ili
kuishinda.

 

“Vita dhidi ya virusi vya Corona ina changamoto kubwa kwa kila mtu na kila mahali. Vitaa hii pia ina gharama kubwa na kwa hiyo ni lazima tuungane. Tusimame pamoja ili tuweze kuokoa maisha yetu na ya ndugu zetu, “ alisema Waziri Ummy.