************************************
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuwa makini katika kuzivaa barakoa pamoja na unawaji wa mikono pia kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wizara ya afya ili kukabiliana na ugonjwa wa virus vya corona ambao ni janga la dunia.
Hayo yamesemwa na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dkt.Catherin Mangali, wakati akipokea vifaa kinga kutoka kwa Mbunge wa viti Maalumu Mhe. Ether Mahawe.
Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo Dkt. Catherin alisema, janga la corona siyo kwa madaktari pekee bali ni janga la kila mmoja hivyo namkushukuru mbunge huyo kwa msaada wa vifaa kinga ili kukabiliana na virus hivyo.
Kwa upande wake Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Manyara Mhe. Ester Mahawe kwakushirikiana na umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Babati mjini wameweza kukabidhi vifaa kinga kwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Manyara ikiwa ni pamoja na Mandoo 20 kwaajili ya kunawia, lita 50 ya sabuni pamoja na barakoa pc 500 na kusema kuwa lengo la msaada huo ni kwaajili ya wangojwa wa wanafika hospitalini hapo ili kujikinga virusi vya corona.
Naye mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi wilaya ya Babati mjini [UWT] Bi. Gaudina Eddan Hauli amesema kwa wakati huu madactari na wauguzi wapo katika hatari kubwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona kutokana na mazingira ya kazi zao kwani hukutana na watu tofautofauti wakati wa kutoa huduma kwa wangonjwa hivyo nakuiomba jamii kuendela kumomba mungu ili maambukizi yasiendelee kutokea.