************************************
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Mama Queen Mlozi, amezindua ushonaji wa Barakoa (Mask) katika Chuo cha Mafunzo Ihemi cha CCM Mkoani Iringa.
Mama Queen Mlozi amefanya Uzinduzi huo leo tarehe 25 Aprili, 2020 akimuwakilisha Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally.
Katibu Mkuu wa UWT, akizundua utengenezaji huo wa Barakoa, ameeleza kuwa,
“CCM imeamua kutengeneza barakoa kwa bei nafuu, kulinganisha na bei za maeneo mengine ili kutoa huduma na kuwasaidia wananchi kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona ikiwa ni jitihada za kuunga mkono mapambano ya kuutokomeza ugonjwa huo.”
Ameongeza kwa kuwaomba wananchi kote nchini kununua barakoa zinazotengenezwa katika kiwanda hiko cha Ihemi, kutokana na bei nafuu ya shilingi elfu moja tu, zikizingatia ubora na viwango vinavyohitajika na mamlaka za viwango nchini.
Kwa sasa kiwanda hiko kinauwezo wa kuzalisha barakoa takribani elfu 4000 kwa siku na uzalishaji unaongezeka kulingana na mahitaji ya wananchi.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa UVCCM Mwl. Raymond Mangwala na viongozi wengine wa Chama na Serikali Mkoa wa Iringa.