Home Burudani Diamond atangaza kuzilipia kodi familia 500 zilizoathirika na Corona kwa miezi mitatu...

Diamond atangaza kuzilipia kodi familia 500 zilizoathirika na Corona kwa miezi mitatu kila familia

0

*********************************

Msanii wa mizki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ametangaza kuwalipia kodi watu 500 walioathirika na Corona kwa miezi mitatu kila mmoja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameandika ujumbe huu.

“Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususan upande wa biashara….nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo Magumu kwa wengi wetu…ijapokuwa na mimi ni Miongoni mwa walio ndani ya janga hili, lakini nimeona walau kwa kidogo changu nilicho nacho, nitoe kusaidia kulipia kodi za Nyumba kwa miezi Mitatu mitatu kwa familia 500, walau kusaidiana Katika kipindi hiki kigumu cha kupambana na Virusi hivi vya Corona…Licha ya kuwa Tiafa moja lakini siku zote mmekuwa Familia yangu kupitia Muziki wangu, hivyo naamini Shida yenu ni yangu, na Tabasamu lenu ni Langu pia….Jumatatu nitaweka rasmi Utaratibu wote wa namna gani Familia Hizi Miatano zinaweza kupata kodi hizo ya Nyumba….