Mkurugenzi
wa Kiwanda cha Husseini Plastic Industries Limited cha Jijini Tanga,
Yusuph Hassanali kushoto akizungumza na waandishi wa habari mara baada
ya kukabidhi msaada huo
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha Husseini Plastic Industries Limited cha Jijini Tanga,
Yusuph Hassanali kulia akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Martine Shigella kushoto wakati wa makabidhiano ya msaada huo
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha Husseini Plastic Industries Limited cha Jijini Tanga,
Yusuph Hassanali kulia akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Martine Shigella kushoto wakati wa makabidhiano ya msaada huo
WATANZANIA
wenye uwezo wametakiwa kuwa mstari wa mbele kusaidia katika mapambano
dhidi ya Ugonjwa wa Corona kwa kutoa msaada mbalimbali itakayosaidia
kukabiliana nao.
Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Husseini Plastic Industries Limited cha Jijini Tanga, Yusuph Hassanali
mara baada ya kukabidhi msaada wa matenki 5 yenye lita 500 kwa Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Martine Shigella ikiwa ni hatua ya kuunga mkono juhudi za
serikali kupambana na ugonjwa huo.
Alisema kwamba waliamua kutoa
msaada huo baada ya kupita maeneo mbalimbali kuona kuna mkusanyiko wa
watu kutokana na uwepo wa ndoo zenye lita 20 hivyo alipoona hali hiyo
akaona upo umuhimu wa kuweza kutoa msaada huo.
Aidha alisema
kwamba iwapo wakihitaji matenki mengine wameongeza kusaidia matenki ya
lita hizo huku wakiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia juhudi za
serikali kupambana na ugonjwa huo.
“Lakini pia niwatake watu
wengine kulisaidia Taifa kwa kutoa msaada kwani ugonjwa huo umeleta
athari kubwa kwa wananchi “Alisema
Hata hivyo alisema hivi sasa
wao wameanza kuchukua tahadhari wakati wakiwahudumia wateja dukani kwao
kwa kukaa umbali wa mita sita na hata kwenye eneo la biashara wana
wahudumui wateja mmoja au wawili.
Mkurugenzi
huyo aliwataka wakazi wa Mkoa wa Tanga wenye uwezo waweze kuwa mstari
wa mbele na sio mpaka wasubirie waombwe badala yake wahamasike kusaidia
kwenye mapambano dhidi ya Corona