****************************
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,amewaasa wananchi kuacha mzaha na kupuuzia kufuata elimu inayotolewa na wataalamu wa afya kujikinga na ugonjwa wa Corona huku akiwahimiza kuendelea kuchukua tahadhari .
Aidha amewahimiza kutumia kuvaa Barakoa wanapokwenda katika Ofisi mbali mbali za Umma na Binafsi ikiwemo Ofisi yake, kwenye Daladala, Bodaboda na maeneo ya Biashara ikiwemo Sokoni,
Ndikilo alisema tayari Mkoa una wagonjwa watatu na Mkoa huo upo karibu na Dar es salaam penye wagonjwa wengi hivyo wananchi wajilinde kwa kuchukua tahadhari muhimu.
Ndikilo aliyasema hayo katika ziara fupi Wilayani Kibaha (Sokoni, Stendi na Maeneo ya Biashara) iliyolenga kukagua utekelezaji wa tahadhari zinazotolewa katika Kuthibiti maambukizi ya Virusi vya corona.
Pamoja na hayo, aliwahimiza wananchi kunawa kila mara kwa Maji tiririka na sabuni ama kutumia vitakasa mikono,kuepuka mikusanyiko,matamasha ya mziki,kukaa umbali wa mita moja na mwezio, na kutoa taarifa pale wanapohisi kuwa wanadalili za maambukizi ya Virusi vya Corona.
Katika hatua nyingine CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo kimewataka wanachama wa chama hicho kutopuuzia ugonjwa hatari wa CORONA, kwani upo na unasababisha vifo.
Katibu wa CCM wilayani hapo, Salumu Mtelela “;:Nitumie nafasi hii kuwakumbushia wana-Bagamoyo wenzangu, pasipokujali itikadi zetu za kisiasa, tujihadhali kwa ugonjwa huu wa CORONA ambao unaenea kwa kasi, tena unaambukiza kwa njia ya hewa, tuzingatie ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya,