Home Biashara Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation yakabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni...

Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation yakabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 300 kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili kupambana na ugonjwa wa Covid-19

0

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Shaaban Seif Mohammed wanaonekana kwenye Skrini wakiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia wakati kampuni ya Vodacom Tanzania PLC walipokabidhi kiasi cha shilingi milioni 300 kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo ili kupambana na kudhibiti ongezeko la virusi vya Corona visiwani humo. Makabidhiano hayo yalifanyika kwa njia ya mtandao

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (kulia) akipunga  mkono kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (haonekani pichani) wakati akikabidhi kiasi cha shilingi milioni 300 kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar zilizotolewa na kampuni ya Vodacom leo ili kupambana na kudhibiti ongezeko la virusi vya Corona visiwani humo, ambapo walifanya makabidhiano kwa njia ya mtandao. Pembeni ni Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia