Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Shaaban Seif Mohammed wanaonekana kwenye Skrini wakiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia wakati kampuni ya Vodacom Tanzania PLC walipokabidhi kiasi cha shilingi milioni 300 kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo ili kupambana na kudhibiti ongezeko la virusi vya Corona visiwani humo. Makabidhiano hayo yalifanyika kwa njia ya mtandao
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (kulia) akipunga mkono kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (haonekani pichani) wakati akikabidhi kiasi cha shilingi milioni 300 kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar zilizotolewa na kampuni ya Vodacom leo ili kupambana na kudhibiti ongezeko la virusi vya Corona visiwani humo, ambapo walifanya makabidhiano kwa njia ya mtandao. Pembeni ni Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia