Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Matinga,akizungumza
Mtoto wa kiume akiuza mchicha katika soko la Mpanda Hotel
………………………………………………………………………
Baadhi ya watoto wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wanaendelea kujishughulisha na biashara; licha ya serikali mkoani humo kutoa amri ya watoto kutokufanya biashara; ili kuwakinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayojulikana kama korona
Mwandishi wa habari hii amepita katika masoko mbalimbali ya Manispaa ya Mpanda na kuwakuta watoto kadhaa wakifanya biashara mbalimbali
Wapo watoto waliokuwa wakiwasaidia mama zao kupanga mafungu ya mboga, wengine walikuwa na malimau, huku wengine wakiuza mitumba
Walipoulizwa kuhusiana na uwepo wao masokoni na tahadhari ya kujikinga na korona wengi wao walionyesha mizaha huku wengine wakidai kuwa wametumwa na wazazi wao
Mama Halima Kishawi ambaye ni mfanyabiashara wa mboga wa soko la Mpanda hoteli alisema kuwa hana mtu mkubwa wa kumwacha nyumbani hivyo analazimika kufanya biashara akiwa na watoto wake wawili, mmoja mwenye umri wa miaka minne na mwingine mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu
Aidha wafanyabiashara wengine wamezungumzia hali hiyo ambapo wamesema kuwa watoto wanapaswa kupewa uangalizi wa hali ya juu ili kuwakinga na korona
“Sio vizuri hizi biashara wangebeba wazazi wenyewe na sio kumtuma mtoto” alisema Justine Wangabo ambaye ni fundi cherehani katika mnada wa majengo
Bwana Hosea Cheyo ni mmoja wa wazazi wa mkoa wa katavi
amesema ipo haja ya wazazi kuona umuhimu wa kuwakumbusha watoto kujisomea kuliko kuwaacha wakicheza tu siku nzima
“Kwanza niwapongeze walimu wa baadhi ya shule wamekuwa wakitoa majaribio wanafunzi wanafanya; ila sasa na sisi wazazi tufanye majukumu yetu ya malezi bora, unakuta mzazi ni mvivu hata kumfuatilia mtoto! alisema Cheyo
Dokta Yustina Tizeba ni daktari bingwa wa watoto mkoa wa Katavi amewashauri wazazi kufuata ushauri wa wataalamu badala ya kuwaachia
watoto kuzurura hovyo
Kupitia mkutano na viongozi wa dini Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga aliwataka wazazi kuongeza umakini na kuwalinda watoto
Kuna vitoto vidogo ambavyo hata havijielewi vyenyewe ni kucheza tu, kutoka nyumba hii kuhamia nyumba ile, hivi ni vya kufungia ndani vicheze ndani kwao sio kuzurura” alisema Matinga
Pia alitoa onyo kwa wazazi wanaotuma watoto kufanya biashara mitaani kama kuzungusha vitumbua, mafagio