…………………………………………………………………………………..
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
Katika jitihada za kuunga mkono Serikali katika vita dhidi ya homa ya Corona Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa amekabidhi ndoo 100 za kuwawia mikono pamoja na sabuni,vyenye thamani ya milioni mbili ili kujikinga na Corona.
Ndoo hizo pamoja na sabuni zimekabidhiwa katika Kituo cha Afya cha Mlandizi ili zisambazwe kwenye vituo vya Afya, Zahanati zote ,kwa wafanya biashara sokoni pamoja Standi ili kupambana na homa ya Corona.
Jumaa aliwataka wananchi wa Jimbo la Kibaha Vijijini kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa homa ya Corona kwani ni hatari na kuendelea kufuata maelekezo ya Serikali kupitia Wiazara ya Afya katika kujikinga na Corona.
Wakati huo huo,Jumaa alikabidhi kiti mwendo kwa mtu mwenye ulemavu mkazi wa Jimbo la Kibaha Vijijini ili kiweze kumsaidia katika kutembelea na kufanikisha shughuli zake za kila siku.
Wakati huo huo, Jumaa alimuunga mkono kwa vitendo, diwani wa Kata ya Mlandizi Euphrasia (Mama Ndesi) kwa jitihada anazozifanya kwenye Kata yake kwa kujenga Ofisi za CCM za Matawi katika Kata hiyo.
Kwasasa Diwani wa Mlandizi amefanikiwa kumaliza Ujenzi wa Ofisi mbili za Ccm za Matawi ambazo zipo katika hatua ya kupaua, Matawi hayo ni Tawi la Upendo pamoja na Mshikamo.
Jumaa alimuunga mkono kwa kumpatia Bati 15 ili kufanikisha hatua iliyobaki ili Ofisi hizo ziweze kutumika.
Mama Ndesi amekuwa Diwani wa mfano katika kata yake amehakikisha katika kipindi chake cha uongozi kila tawi linakuwa na Ofisi yaani Ofisi za Ccm Tawi ndio maana kwa Jitihada zake kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini ,Jumaa amefanikiwa kujenga ofisi za Ccm za Matawi katika Kata ya Mlandizi.