Home Mchanganyiko ASHIKILIWA KWA KUMPA UJAUZITO MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA

ASHIKILIWA KWA KUMPA UJAUZITO MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA

0

…………………………………………………………………………….

Na Masanja Mabula ,PEMBA

JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba limashikilia kijana khamis shaib khatib 24 anayetuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 13.

Akizungumza Ofisini Kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba ,Kamishina Msaidizi mwandamizi Juma Sadi Khamis alisema kijana huyo ambaye alikuwa kwenye harakati za kukimbia kwa sasa anashikiliwa na jeshi hilo akisubiri upelelezi ukamilike ili fikishwe Mahakamani.

Alisema jeshi la polisi kwa kushirikiana na wasamaria wema wamefanikiwa kupatikana mtuhumiwa huyo baada ya kutoa taarifa sahihi zilizofanikisha kumtia mikononi.

“Nawashukuru sana waliofanikisha kupatikana mtuhumiwa huyu, tunaendelea kumhoji na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani “alisema.

Aidha Kamanda Sadi aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na kuwa tayari kwenda kutoa ushahidi mahakamani wanapohitajika.

“Nawaomba sana wananchi wawe tayari kwenda kutoa ushahidi mahakamani ili mahakama ipate vielelezo ambavya vitasaidia mtuhumiwa kutiwa hatiani”alieleza.

Mwalimu Mkuu Skuli ya Msingi aliyokuwa akisoma msichana huyo, Said Juma Kombo (sio jina lake sahihi) alikiri kupokea taarifa za mwanafunzi huyo kuwa na ujauzito.

Alifahamisha kwamba mwanafunzi huyo alikata  kuhudhuria masomo kabla ya skuli kufungwa , kutokana na kujibaini kwamba ni mjamzito.

 

Naibu Sheha  Riziki Rashid alisema usiri ulitumika baina ya viongozi wa Shehia na Jeshi la Polisi hadi kufanikisha kumkamata kijana huyo

Baadhi ya wananchi waliiomba Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya mtuhumiwa huyo.

Walisema katika suala hili ni lazima serikali kusimamia ili kuzuia kufanyika suluhu kwani itakuwa ni kumjengea mazingira magumu mtoto wa kike.

“Anakiruhusiwa  kumuoa naamini hatakaa naye kwani itakuwa anakimbia kifungo mahakamani , hivyo naomba hili lisipewe nafasi”alisema mmoja wa majirani.

Kwa sasa msichana huyo anaishi wa naibu sheha , ambapo wanahofu kwamba kuvurugwa ushahidi na mtoto kuolewa.