Didier Drogba ameitoa hospitali yake nchini Ivory Coast itumike kama kituo cha matibabu ya wagonjwa wa virusi vya corona PICHA ZAIDI SOMA HAPA
………………………………………………………………………..
NYOTA wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba ameitoa hospitali yake nchini Ivory Coast itumike kama kituo cha matibabu ya wagonjwa wa virusi vya corona.
Hospitali hiyo iliyopo Abidjan – ilifunguliwa mwaka 2016 na imepewa jina la gwiji wa soka wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Pokou, aliyefariki dunia mwaka huu ilipofunguliwa.
Kwa sasa ugonjwa wa COVID-19 bado haujawa tishio kubwa barani Afrika, ingawa kuna wasiwasi baadaye virusi hivyo vitasambaa kwa wingi zadi.
Mkuu wa Mkoa wa Abidjan, Vincent Toh Bi Irie amemshukuru sana Drogba kwa msaada huo wa kibinadam na amesema kwamba hospitali hiyo itasaidia katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Hospitali hiyo ya Ivory Coast ni sehemu ya Mfuko wa Didier Drogba ambaye enzi zake aliifunga mabao 65 nchi yake katika mechi 105, aliouanzisha kukusanya fedha za kusaidia afya na elimu Afrika.