Home Mchanganyiko SIO SERA YA CHINA KURIDHIA UBAGUZI-BALOZI MBELWA

SIO SERA YA CHINA KURIDHIA UBAGUZI-BALOZI MBELWA

0

*****************************

NA EMMANUEL MBATILO

Serikali ya China haiwezi kukubali vitendo vyovyote ambavyo vina malengo ya kuzalilisha utu wa mtu yoyote kufanyika nchini humo.

Ameyasema hayo Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa Kairuki baada ya kukutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Chen Xiaoding na kuelezea taarifa zinazosambaa kuhusu Waafrika katika nchi ya China kutengwa.

Akizungumza hivi karibuni amesema kuwa alipokutana na Naibu Waziri aliwaelezea masuala mbalimbali ikiwemo taarifa inayozagaa mitandaoni kuhusu masuala ya kutengwa kwa Waafrika katika nchi hiyo ya China kutokana na Maambukizi ya Virusi vya Covid-19.

“Naibu Waziri alitupa maelekeze ya ziada kuhusu masuala kadhaa ambayo yameonekana kwenye mitandao ya kijamii na moja ya mambo ambayo aliyaelezea ni lile suala la Waafrika ambao wapo kwenye mji wa Guangzhou kulazimika kupimwa Covid-19 kwa lazima”. Amesema Mhe.Mbelwa.

Aidha Mhe.Mbelwa amesema kuwa Naibu Waziri aliwaeleza uamuzi huo wa kuwapima umetokana na mambo matatu ambapo serikali ya Guangdong imeyabaini ambayo moja wapo lilibaini wanaotoka nje au kuja katika jimbo la Guangdong kati ya watu 26, 19 walikuwa wanatoka barani Afrika.

Pamoja na hilo amesema kuwa walibaini pia katika kufanya vipimo kwa watu mbalimbali ilidhihirika kwamba watu 60 ambao wanavirusi lakini hawaonyeshi dalili ambapo 57 walikuwa ni waafrika.